Maumivu ya kukosa sheria mpya ya habari Zanzibar.
Na, Thuwaiba Habibu Raha na furaha ya safari ni kufika ulikokusudia kwa salama na amani. Baadhi ya safari huwa ngumi na huwa zenye maumivu na athari nyingi Miogoni mwa safari hizi ni ya waandishi wa habari kutaka kuwa na sheria zenye mazingira bora ya kazi zao. Kwa Takribani miaka 20 sasa waandishi na wadau wengine wa habari wamekuwa wakionyesha vifungu vya sheria ya habri vinavyominya uhuru wa habari na wa kujieleza. Lengo ni kutaka sheria rafiki itakayofanya mazingira ya kukusanya na kutoa habari Zanzibar kuwa rafiki na kuweza kuchangia vizuri maendeleo ya visiwa vya Unguja na Pemba. Lakini kelele hizo zimekuwa kama zile za msemo maarufu wa Kiswahili wa kelele za mpangaji hazimzuwii mwenye nyumba kulala. Zanzibar ilikuwa na historia nzuri na ya kuvutia ya habari na vijana wake kuchangia maendeleo ya sekta ya habri, hasa ya kufungua idhaa za Kiswahili katika nchi mbali mbali duniani. Kutoka zama hizo na hadi leo visiwa hivi vimetoa manguli wa taaluma ya habari kwa nyakati mbali mbal...