NA, HASSAN MSELLEM – PEMBA Waandishi wahabari wachanga Visiwani Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya kutambua taarifa sahihi katika kuelekea Uchanguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 29. 2025. Akifungua mafunzo hayo kwa waandishi vijana kutoka Unguja na Pemba Mkurugenzi kutoka Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Mjini Unguja, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwandaa Waandishi Habari vijana kutekeleza majukumu ya kihabari kwa weledi katika Dunia ya sasa yaliyotawaliwa na matumzi mabaya ya ‘AKILI UNDE’ Aidha Mkurugenzi huyo amewasisitiza waandishi hao umuhimu wa kujifunza matumizi sahihi ya ‘AKILI UNDE’ katika kuhakikisha taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuelewa usahihi wake. “Ngudu waandishi kama munavyofahamu kuwa katika dunia ya leo tumegubikwa na matumizi mazuri na mabaya Artificial Intelligence (AKILI UNDE) hivyo lengo la mafunzo haya kwenu ni kuona ni kwa namna gani mutaweza kutamb...