Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba
Habari Na, Hassan Msellem, Pemba
Picha kutoka Maktaba. |
Mchanga Omar Said anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35, na mama wa watoto saba Mkaazi wa Shehia ya Sizini Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua na kisha kumfukia kwenye tuta mtoto wake Mchanga.
Akizungumza juu ya tukio Hilo Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, alisema majira ya saa 5 siku ya Tarehe 18\05\2024 wamepokea taarifa za mama huyo akiwa na ujauzito ambalo alijifungua bila ya taarifa za alichojifungua kuonekana, ndipo Wananchi walipofuatilia na kugundua kuwa mama huyo alijifungua na kisha kumuua mtoto na kisha kukizika.
Akizungumza kwa niaba ya mganga Mkuu wa hospital ya Micheweni Daudi Rashid Mkasha, alisema walipofika eneo la tukio walikuta sehemu iliyochumbuliwa na kukuta mabaki ya mwili wa mtoto ambayo tayari yameshaharibika.
Suleiman Shaame Hamad, ni Sheha wa Sizini alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuhuzunishwa nalo pamoja na kuwataka Wananchi kuachana na vitendo vya ukatili.
Inasemekana baada ya mama huyo kugundua kuwa Wananchi wameshapata taarifa za tukio alilonitenda alianza kuchukua hatua za kujinyonga lakini Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumtia mbaroni.
Ni ukatili uliopitiliza kwakweli, mtu na akili timamu unafanya ushetani wako kisha unaenda kukihukumu kiumbe ambacho hakina makosaðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜
ReplyDelete