Kamati za mazingira za Shehia kisiwani Pemba zimetakiwa kuielimisha jamii juu ya masuala ya haki yanayotokana na tabia nchi ili kurekebisha athari za mabadiliko hayo. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa mwanvuli wa asasi za kiraiya Zanzibar Hassan Khamis Juma katika hafla ya kujengewa uwelewa wanakamati hao juu ya masuala ya haki yanayotokana na tabia nchi huko madungu chake chake Pemba. Amesema ikiwa dunia ipo katika janga la mabadiliko ya tabia nchi ni vyema wananchi kwa kushirikiana na kamati kuchanganua haki zao ili kuweza kupata mbinu za kupunguza madhara yanayojitokeza Kwa upande wake Mwalimu Khamis Mwalimu kutoka idara ya mazingira Pemba amesema ni vyema kamati za shehia kuitunza na kuilinda miundombinu iliyowekwa katika shehia zao ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi Naibu katibu wa mwenvuli wa asasi za kiraiya Pemba Alawi Bakari amesema maeneo mengi Tanzania yameshaharibika kutokana na mabadiliko ya labia nchi hivyo ni vyema kushirik...