Habari Na, Zuwena Shaabani Pemba
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika Ajali aliyohusisha gari ya abiria aina Dyna ruti Nambari 602 yenye namba za usajili EK 189 na vyombo vya maringi mawili aina ya Vespa katika Eneo la Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Wakizungumzia ajali hiyo mashuhuda walisema, walishuhudia kugongana kwa gari hizo baada ya kusikia mshindo mkubwa ambao ulipelekea mtu mmoja kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Richard Tadeo Mchomvu alisema ajali hiyo ilitokana na kugongana uso kwa uso kati ya gari aina ya Dayna na ya mizigo Fuso na kupelekea gari hiyo iliyokuwa na abiria zaidi ya 30 kupinduka.

Comments
Post a Comment