Skip to main content

Waandishi wa habari watakiwa kuwashajihisha wanawake kuingia kwenye michezo.

 Na Nihifadhi Abdulla, Zanzibar.


WAANDISHI wa habari wametakiwa kuwashajihisha wanawake kuingia kwenye michezo huku wakizigatia maadili na silka za Kizanzibari kwa kujiheshimu na kulinda hadhi yao


Yamesemwa hayo na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Dk Mzuri Issa wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kushajihisha wanawake kushiriki kwenye michezo yaliyofanyika katika Ofisi za  TAMWA  Mkoa kusini Unguja.

 

Amesema waandishi wananafasi kubwa ya kusikilizwa kwenye jamii hivyo ni vyema kwenda kuyatendea kazi wanayoelekezwa ili lengo liweze kufikiwa


Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya TAMWA   Bi  Hawra Shamte amesema kuna mitazamo mbalimbali katika jamii zinamkwamisha mwanamke kushiriki michezo hivyo anaimani waandishi wakitumia kalamu zao vizuri kuelimisha jamii dhana ya michezo kwa maendeleo itapatikana


Amesema uwepo wa sera ya Michezo  ya mwaka 2018 ni kielelezo kuwa  Serikali inazingatia sekta hiyo na inaendelea kuweka mikakati katika kushughulikia tofauti za kijinsia kwa maendeleo ya taifa 


Nae mtaalam wa michezo kutoka Shirika la maendeleo  la Ujerumani (GIZ) Makame Amir Mgeni Amesema ni wakati sasa jamii kuelimishwa kumruhusu mwanamke kushiriki kwenye  Michezo kwani inafaida kiafya, mwili na akili. 


Mradi wa Michezo kwa maendeleo unaolenga kukuza usawa wa kijinsia katika sekta hiyo unatekelezwa na TAMWA ZANZIBAR, Kwa kushirikiana na Shirika la GIZ.



Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...