NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Mahakama ya Kupambana na Makosa ya Udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake, Jana April 14 imemuhukumu kutumikia Chuo cha Mafunzo Ismail Ussi Makame miaka 19, mkaazi wa Mikarafuuni kwa makosa mawili ya Ubakaji. Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Taki Abdalla Habib, imeelezwa na mwendesha Mashtaka Asia Ibrahim Mohamed, kuwa tarehe 19.12.2025 saa 7:00 za usiku huko Kinyasini Mkoani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, mshtakiwa alimbaka msichana wa miaka 16 baada ya kumtorosha msichana huyo kutoka nyumbani kwao na kwenda nae sehemu anayolala, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 108(1)(2) na 109(1) Shehia ya adhabu Sheria Nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar likiwa ni kosa la kwanza. Katika kosa la pili, tarehe 20.12.2025 saa 7:30 za usiku mshtakiwa alimbaka tena msichana huyo. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mahakamani hapo 06.01.2026 na idadi ya mashahidi 6 walitoa ushahidi ambao haukuacha chembe ya shaka, hivyo Mahakama...
HABARI, NA HASSAN MSELLEM. Baada ya zaidi ya miongo miwili ya kujitolea, uongozi na harakati za kutetea haki za wanawake, watoto na uhuru wa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania, Tawi la Zanzibar (TAMWA–ZNZ), Dk. Mzuri Issa Ali ameaga rasmi waandishi wa habari kutokana na kuondoka katika wadhifa wake, akiacha taasisi imara yenye mifumo thabiti na mafanikio yanayotambulika kitaifa na kimataifa. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wanachama wa TAMWA–ZNZ, Mkurugenzi huyo amesema waandishi wa habari ndio nguzo kuu ya taasisi hiyo licha ya changamoto kubwa wanazokumbana nazo lakini bado waliendelea kushirikiana na Tamwa Zanzibar katika kutumia kalamu zao kuelezea harakati za shughuli za Tamwa Zanzibar. “Kama kuna kundi la watu wanaojua kuuliza maswali magumu, kufuatilia ukweli bila kuchoka, na bado malipo yakawa madogo au hakuna kabisa, basi hao ni waandishi wa habari. Na cha kufurahisha zaidi, hao ndio ngu...