Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MICHEZO

"AMINA" KINARA WA UOGELEAJI BONANZA LA UTALII PEMBA

 NA, SALIM FAKI, PEMBA "AMINA" KINARA WA UOGELEAJI BONANZA LA UTALII PEMBA Na, Hassan Msellem, Pemba Ni msichana wa miaka 15, Mkaazi wa Tumbe Mashariki anayesoma kidato cha Pili aliwashangaza wengi walioshiriki mashindo ya mchezo wa kuogelea yaliyofanyika huko Vuma Wimbi katika Pwani ya Msuka Kaskazini mwa Kisiwa Cha Pemba kwa kipawa chake cha kupiga mbizi na kuwashinda wapiga mbizi wenzake 14 na hatimae kuibuka mshindi wa pili. Msichana huyo mwenye umri mdogo zaidi kuliko waogeleaji wote walioshiriki mchezo huo aliwaacha vinywa wazi watu wote waliokuwa wakishuhudia mtanange huo wapasua maji pasi na msaaada wowote wa waongoza mashindano hayo yaliyojumuisha urefu wa mita 20 Baada ya ushindi huo mwandishi wa Makala hii alipata nafasi ya kuzungumza na msichana huyo ilikufahamu siri ya kuibuka mshindi wa pili na kusema kufanya mazoezi kwa bidii ndio siri pekee iliyofanya awe na uwezo wa kupasua mawimbi zaidi kuliko wenzake ambao walionekana mapafu yao kukomaa zaidi na kwa...

GHARAMA ZA VIFAA VYA MICHEZO, KIKWAZA KWA WANAWAKE KUSHIRIKI MICHEZO.

 N A, SALIM HAMAD, PEMBA Gharama za Vifaa vya Michezo ni miongoni mwa kikwazo kinachowafanya wanawake kushiriki michezo mbali mbali Kisiwani Pemba. WAKATI Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi mbali mbali za kiraia nchini ikiwemo Chama Cha Waandishi wa Habar wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA) zikielekeza nguvu zake katika kuhamasisha wanawake kushiriki michezo, ingawa bado kumekuwa na kikwazo katika upatikanaji wa vifaa vya michezo. Michezo ni jambo zuri ambalo limekuwa na umuhimu wa kipekee katika kuimarisha afya za wananchi. Pia michezo ni suala ambalo serikali na wadau wengine wamekua wakielekeza nguvu zao na kuekeza katika sekta hiyo, hivyo imekua ni kichocheo kikubwa cha kupata fursa ambazo zinaweza kuinua uchumi wa wanamichezo. Kutokana na umuhimu wa michezo hata jukwaa la Beijing kupitia mkutano ulioandaliwa na shirika la UN Women likishirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, wakati wa vikao vya 59 vilitambua pia umuhimu wa michezo na elimu ya mazoezi ya mw...

WASEMAJI WANAWAKE KWENYE TIMU WAONGEZA HAMASA MICHEZONI.

Na Amina Mchezo  Uhamasishaji michezoni unatokana na uwepo  wa watu maalum ambao hutumia muda wao mwingi kutafakari namna gani ya kuwaleta watu karibu na Kwa mbinu gani. Michezo kikawaida huhitaji mvuto mkubwa Kwa jamii kwani uwepo wake huleta furaha na kujuana na watu mbalimbali. Maafisa habar i kwenye michezo wananafasi kubwa ya kutoa taarifa zinazohusu vilabu na wanachama wengine. Inaelezwa kuwa ili upatiwa leseni ya timu yako na shirikisho la mpira wa miguu ni lazima uwe umetimiza vgezo ikiwemo kipengele Cha kuwa na afisa habari wa timu. Huku cha kusikitisha zaidi ni Kuona timu ambazo zinategemewa kibeba Zanzibar hata hawaoni umuhimu. kuwa na afisa habari. Hadi Sasa maafisa wa habari wanawake katika michezo ni wawili tu Kwa Zanzibar huku Timu Zote 16 znazoshiriki ligi kuu Zanzibar hakuna timu yenye msemaji mwanamke, wakati ligi daraja la kwanza Kanda ya unguja timu Moja tu kati ya timu 18 ndio yenye msemaji mwanamke na timu Moja tu ilio mkoa ndio yenye msemaji mwanamke....

"Tuhamasishe watoto wa kike kushiriki michezo kuleta usawa wa Kijinsia katika sekta zote" Afisa Programu Tamwa, ZNZ

Na, Thuwaiba Habibu, Unguja Katika kuazimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike duniani, wadau wa michezo kwa maendeleo Zanzibar ambao ni Jumuiya ya wanasheria wanawake, Zanzibar (ZAFELA) kituo cha mijadala kwa vijana (CYD)na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,ZNZ) kwa kushirikiana na shirika la Ujerumani (GIZ) imeandaa shughuli mbali mbali za michezo kwa maendeleo ili kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike na ustawi wa kijinsia katika michezo. Akitoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari Afisa Program wa michezo kwa maendeleo kutoka Tamwa Zanzibar, Khairat Haji amesema maadhimisho hayo yatawashirikisha wanafunzi kutoka skuli mbali mbali za msingi za mkoa wa kaskazini 'A', Mjini ,na Magharibi 'A', na yataanza kwa michezo ya mpira wa pete (Netball) za kirafiki zitakazo husisha timu za watoto wa kike kutoka tumbatu, jongwe,mkokotoni,mto wa pwani, kianga,mtoni , kiembe samaki B' na uroa. Alisema kuwa shughuli nyengine zitakazo ...

“SMILE PEMBA MARATHON” KUBORESHA USTAWI WA WATU WENYE ULEMAVU

  Na, Hassan Msellem- Pemba Wananchi Kisiwani Pemba wametakiwa kushiriki mashindano ya Mbio yanayobeba jina la Smile Pemba Marathon ili kufanikisha lengo la Mbio hiyo. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Ahmed Abuubakar Mohammed huko Gombani Pemba, amesema lengp la Mbio hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba na vifaa saidizi kwa watu Wenye Ulemavu. Aidha amesema Mbio hizo za hisani zinatarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024, katika Uwanja wa Gombani Pemba kwa kukusanya wanariadha kutoka ndani na nje ya Nchi, ambapo Mgeni rasmi wa mbio hizo anatarajiwa kuwa makamo wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla “Naomba nitowe wito wangu kwa wananchi Watanzania wote wapenda maendeleo kuweza kushiriki katika mbio hizi na pia kuweza kutoa michango yao kwa ajili ya kusaidia Watu Wenye Ulemavu” amesema Aliongeza kuwa Mbio hizo zinatarajiwa kuwa mbio za Nusu Marothon zikijumuisha mbio za Kilometa...

“Nimeshiriki michezo tangu nikiwa darasa la tatu kwasasa ni kocha wa timu ya wanawake ya mpira wa miguu maadili yangu ya Kizanzibari yako pale pale” Tamasha Kocha wa timu-Wete Women Club

  Makala Na, Hassan Msellem-Pemba Mpira wa Miguu au wengi wanapenda kuita Soka, Kandanda, Ndinga au Kabumbu yote yakiwa ni majina sahihi kwa mujibu wa wapenzi wa mchezo huo.  Unachezwa uwanjani ukiwa na jumla ya wachezaji 22 kila timu ikiwa na wachezi 11, lengo la mchezo huu ni wachezaji kumiliki mpira kwa kutumia miguu kwa shebaha ya kufunga goli yani kuingiza mpira kwenye wavu zilizosimamishwa kwenye milingoti mitatu yani kulia, kushoto na juu. Inakadiriwa kuwa mnamo karne ya 21, kulikuwa na wachazaji mpira wapatao milioni 250 kati ya watu bilioni 1.3 Duniani. Mwaka 2010 hadhira ya televisheni ya zaidi bilioni 26 ilitazama mashindano ya kwanza ya kombe ya Soka, fainali za Kombe la Dunia za mwezi wa nne. Licha umaarufu nakupendwa kwake hakukuwa na timu za wanawake na hii nikutokana na asili ya mchezo huo kuchezwa na wanaume huku baadhi ya mataifa kutokana na Mila na Tamaduni zao wakiami wanawake kushiriki katika mchezo huo ni kwenda kinyume na mil ana tamaduni zao. Laki...

Kukosekana Udhamin ligi za wanawake wadumaza maendeleo ya michezo.

Na, Amina Mchezo. Udhamini ni chachu ya kulifanya jambo au shughuli Kwa urahisi na Kwa uhakika wa hali ya juu. Udhamini inategemea na namna ya makubaliano yenu haijalishi iwe fedha, ama bidhaaa au vifaa ilimradi unahakikisha unafanya jambo lako likiwa na usimamizi kamili. Udhamini katika michezo unatoa fursa na hamasa ya wachezaji kuona Wanapata heshima na kuwekewa sawa maslahi yao pamoja na clabu yao. Wadau mbalimbali wa michezo wamesema timu za wanawake hazina udhamini kutokana na kukosa mvuto  kutokana na wanawake wengi Kwa Zanzibar hawana mwamko wa kimichezo. Wameendelea kusema kuwa Kwa Zanzibar wanawake kucheza mpira imekuwa na mitazamo tofauti na ndio maana wadau wengi wanashindwa kuwekeza fedha zao katika timu au ligi za wanawake. Wakizungumza na mwandishi wa makala hii wadau hao wamesema udhamini wowote unatakiwa uwe na faida pia Kwa pande Zote huku mdhamini akitumainia kutangaza biashara, taasisi au kampuni yake. "Unajua Kila kitu ni mwamko wa watu uwanjani na ndio unaosa...

TAMWA ZNZ, ZAFELA, CYD na GIZ waipongeza Timu ya WARRIOR QUEEN kushiriki mechi ya Klabu Bingwa Afrika, Ethiopia.

Watekelezaji wa program ya Michezo kwa Maendeleo Zanzibar (S4D) wanawatakia kila la kheri timu ya Warrior Queens ya Saateni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yanayotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 31 Agosti mwaka huu 2024. Timu ya Warrior Queens itaiwakilisha Zanzibar katika mashindano hayo na inatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Ethiopia siku ya Alkhamis, tarehe 15 Agosti 2024. Tunaamini kuwa wataiwakilisha Zanzibar kwa fahari kubwa na kurudi nyumbani wakiwa washindi. Pamoja na kuwapongeza wadau wote waliofanikisha timu hii kukamilisha mahitaji ya safari hiyo, TAMWA ZNZ inasisitiza umuhimu kwa wadau wote kuendeleza usawa wa kijinsia kwa kuzisaidia timu za wanawake na kukuza vipaji vyao ili kujenga jamii inayothamini na kuinua michango ya wanawake. Bado ipo haja kwa wadau wote wa michezo, ikiwemo serikali, taasisi binafsi, na wadau wengine, kuongeza...

Elimu na miundombinu rafiki inahitajika katika kukuza ushiriki wa jinsia zote katika michezo- Tumbatu

  SHEHA wa Tumbatu Uvivini ndugu Ngwali Sheha Haji, amesema miongoni mwa changamoto zinazopelekea kutokuwepo ushiriki sawa wa kijinsia katika michezo ni pamoja na kukosekana kwa miundo mbinu rafiki na skuli kutokua na muda maalum wa michezo kwa wanafunzi. Sheha Ngwali amesisitiza kuwa mila na desturi sio kikwazo kwani historia inaonesha kuwa kuna wanawake mbalimbali kutoka kisiwani hapo ambao wamewahi kushiriki michezo na kuwa vinara katika kisiwa hicho. “Hapo zamani miaka ya 1973 wakati mimi ni mwanafunzi kulikuwepo wanawake wanaoshiriki michezo na kuchukua medali nyingi lakini ushiriki umepungua kutokana na changamoto za ukosefu wa mazingira rafiki ya kushiriki michezo kwa watoto wa kike”, alisema Sheha Ngwali. Nae Mwalimu mkuu msaidizi skuli ya Tumbatu Msingi “A” ameeleza kuwa skuli hiyo ina mikakati ya kuwahamasisha watoto wa kike kushiriki michezo hususan baada ya kukamilika viwanja rafiki vya michezo kupitia mradi wa michezo kwa maendeleo Kwa upande wa wanafunzi wa kike wanao...

"Hata Dini zetu zimehimiza kushiriki michezo Ili kuwa na afya imara" Othman Massoud Othman

Na, Hassan Msellem, Pemba MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, amevishauri vilabu ya mazoezi nchini, kujitengenezea kanuni, zitakazowavutia watu wingi zaidi kujiunga kwenye mazoezi, ili kuondoa dhama potofu ya mazoezi ni uhuni. Alisema, kama kundi kubwa la watu wanadhana kuwa mazoezi ni uhuni na kuvunja maadili, ni wakati sasa kwa vilabu vya mazoezi na michezo, kuwa na kanuni zitakazofuta dhana hiyo. Makamu huyo wa Kwanza, aliyasema hayo leo Julai 28, 2024 uwanja wa michezo Gombani Chake chake, kwenye bonanza la miaka 10, tokea kuanzishwa kwa ‘Gombani Fitness Club’ lilioandaliwa kwa pamoja na TAMWA-Zanzibar na Shirika la Bima. Alieleza kuwa, kwa vile mozoezi ni jambo muhimu kwa kila mmoja, ni vyema kuwepo na kanuni ndogo ndogo, ambazo zitawavutia wengine, kushiriki katika kupata kinga ya miili yao. Alifahamisha kuwa, ni kweli kama kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili, inaweza kuwa sababu kwa baadhi ya watu, kuona sio sehemu salama, ingawa zikiwepo kanuni zitawavut...

BONANZA LA MICHEZO KUIBUA VIPAJI VYA WANAMICHEZO WANAWAKE PEMBA.

Na, Hassan Msellem, Pemba. CLUB ya mazoezi ya viungo Gombani fitness kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar pamoja na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) wameandaa bonanza la michezo na mazoezi Kisiwani Pemba litakaloanza shamra shamra zake kuanzia kesho tarehe 20 na kufikia kilele siku ya tarehe 28.07.2024 huu kwa kufanyika matembezi ambapo zaidi ya washiriki 500 kutoka nje ya kisiwa cha Pemba wanatarajiwa kushiriki katika bonanza hilo. Akizungumza Mratibu wa Bonanza hilo KHalfan Amour Muhamed ambae pia ni Katibu wa Gombani fitness, alisema kuwa lengo Bonanza hilo litakaloanza na matembezi kutoka Madungu hadi uwanja wa Gombani kuanzia saa 12 za asubuhi ni kusaidia kuhamasisha ushiriki wa wanawake na wasichana kwa kushirikisha na kukuza usawa wa kijinsia katika michezo ya aina mbali mbali kwa wanawake kisiwani humo . Amesema Club hiyo kwa kutambua juhudi zinazofanywa na wadau wa michezo kwa wanawake wameona kuna umuhimu mkubw...