Skip to main content

Posts

Showing posts with the label VIJANA

"ZU" YAANDAA MAHAFALI YA 23, DISEMBA 17.2025.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) UNAYOFURAHA KUWAALIKA WAHITIMU WOTE WA MWAKA WA MASOMO 2024/2025, PAMOJA NA WAZAZI, WALEZI, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA ELIMU KUSHIRIKI KATIKA MAHAFALI YA 23 YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU). MAHAFALI HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAATANO 17 MWEZI DISEMBA 2025, KATIKA KIWANJA CHA CHUO KIKUU TUNGUU KIBELE KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI, AMBAPO MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO ANATARAJIWA KUWA RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI. UONGOZI WA CHUO UNAWASHAURI WAHITIMU WOTE KUKAMILISHA TARATIBU ZOTE IKIWA NI PAMOJA NA KUCHUKUWA MAJOHO KUANZIA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 11 HADI TAREHE 15.  MAZOEZI YA MAHAFALI YANI REHASAL ITAFANYIKA TAREHE 16. WATU WOTE WANAKARIBISHWA KATIKA MAHAFALI HAYO. CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) NI CHEM CHEM YA MAADILI NA TAALUMA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SIMU NAMBARI  0714843480/0718321095/0778777878 AHSANTENI

Ongezeko la Madiwani Wanawake Vijana 2025, Tumaini Jipya Wanawake kuwa Viongozi.

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA. Ongezeko la madiwani wanawake katika ngazi mbali mbali Mkoa wa Kusini Pemba limekuwa ishara ya mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, pamoja na mwamko mpya wa jamii kutambua uwezo wa wanawake kama viongozi bora na chachu ya maendeleo. Miongoni mwa Madiwani Wanawake vijana waliopata fursa ya kuteuliwa kushika nafasi hizo na kuwawakilisha Wanawake wenzako vijana ni pamoja Amria Seif Saleh, ambaye ameteuliwa kuwa Diwani wa Baraza la Mji Mkoani na Fatma Khamis Ali, ambaye ni Diwani wa Wadi Kibokoni Vitongoji, wote wakiwa ni vijana chipukizi katika ulingo wa siasa na uongozi Kisiwani Pemba. Mabadiliko ya Kijamii na Kuongezeka kwa Uelewa k atika kipindi cha miaka ya karibuni, kumekuwa na kampeni mbalimbali zinazoendeshwa na mashirika ya kiraia, Serikali na taasisi binafsi zinazolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi, Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa usawa wa kijinsia na nafasi ya mwanamke katika maamuzi imechangia kwa kiasi kikubwa kupungu...

MABARAZA YA VIJANA, SIASA NA USHAWISHI SUALA LENYE MAONI TOFAUTI.

Na, Hassan Msellem- Pemba Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chake Chake Zulekha Maulid Kheri Historia ya kuanzishwa kwa Mabaraza ya Vijana ilianza mwaka 1948 katika nchi ya Urusi, ambapo lengo la kuanzishwa kwa mabaraza hayo ni kuwaunganisha Vijana wa maeneo mbalimbali wa Taifa hilo ili kutambuana na kuwa wazalendo wa taifa lao,hasa pale inapobidi kulitetea dhidi ya adui, ikizingatiwa kipindi hicho dunia ilikuwa inakabiliwa na Vita vikuu vya Pili. Huko Kisiwani Pemba Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Salum Issa Ameir, amesema vijana waliojiunga na mabaraza ya vijana katika Wilaya zote za Pemba ni 9,308 wanaume wakiwa 4,754 na wanawake ni 4,553 sawa na asilimia 48% ya vijana wakike waliojiunga na mabaraza hayo, ambapo Wilaya ya Micheweni Vijana wa kiume waliojiunga baraza la vijana ni 1,078 na wanawake wakiwa 952, Wilaya ya Wete wanaume 1,176 wanawake 1,041, Wilaya ya Chake Chake wanaume 1,260 wanawake 1,386 na Wilaya ya Mkoani wanaume 1,240 wanawake 1,174. Idadi inayojumuish...