Skip to main content

“Upatikanaji uhuru wa habari haunufaishi vyombo vya habari tu, bali ni kwa manufaa ya taifa kwa jumla” Dkt. Mzuri Issa


Hassah Msellem



Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Tamwa, Kanda ya Zanzibar Dkt. Mzuri Issa amesema ipo haja ya kufanyia marekebisho sheria ambazo zinakinzana na upatikanaji wa habari na uhuru wa vyombo vya habari ili kuchochea uwajibikaji na upatikanaji wa taarifa kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii.


Amebainisha hayo wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Zanzibar ya kuwajengea uwezo  kutambua mapungufu yaliyopo katika sheria za habari  na kujadili mkakati wa kufanya uchechemzi wa mabadiliko ya sheria hizo ili kuweka mazingira rafiki ya vyombo vya habari Zanzibar.


Ameeleza kuwa suala la upatikanaji wa uhuru wa habari sio suala linalolenga kuwanufaisha waandishi na vyombo vya habari pekee bali ni suala mtambuka lenye manufaa ya kujenga uwajibikaji kwa viongozi na jamii kwa ujumla katika upatikanaji wa huduma.


Akiwasilisha mapitio ya sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu Na. 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria Na. 8 ya mwaka 1997, Imane Duwe, mkufunzi wa habari alisema Kifungu cha 3 cha sheria hiyo kimempa Waziri mamlaka ya kuteua Msajili wa Vitabu na Magazeti lakini iko kimya juu ya sifa na uzoefu wa msajili huyo


Alieleza, “nafasi ya msajili inatakiwa itangazwe na achaguliwe kwa mujibu wa sifa, mfano awe mwanasheria au mtu mwenye taaluma ya habari na mawasiliano ya umma na sifa za msajili zinapaswa kuainishwa katika sheria.”

Aidha alibainisha kuhusu upatikanaji wa taarifa hakuna kifungu kinachozungumzia haki ya muandishi wa habari kupata taarifa kutoka kwa mamlaka mbalimbali.  

Sheria hii hajaweka na kuzingatia uhitaji  wa sasa kulingana na dhana ya kidemokrasia au kuwa ni haki ya msingi kutengeneza mazingira ambayo mwandishi ataweza kupatiwa taarifa na habari pale inapohitajika hivyo tunapendekeza kiwepo kifungu maalum kitakachozungumzia upatikanaji wa taarifa na  habari na kuanisha hatua zitakazo chukuliwa kwa aliyepewa dhamana ya kutoa taarifa hizo pale asipotekeleza haki hiyo,” alifahamisha mkufunzi huyo.

Mkufunzi katika mafunzo hayo Imane Duwe


Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ, Dkt. Mzuri Issa aliwataka waandishi wa habari kuendelea kufanya ushawishi wa mabadiliko ya sheria zenye mapungufu ili kutoa fursa ya upatikanaji wa sheria zinazoweka mazingira bora kwa vyombo vya habari Zanzibar kutekeleza majukumu yake.


Alibainisha mkurugenzi huyo, "haki haiji mezani, ni lazima tukazane, tusiogope sheria na wala tusikate tamaa, tuendelee kuandika kwani sheria zipo kwaajili yetu ilimradi tunachokifanya ni kitu sahihi hatuvunji sheria. Twende tukaandike zaidi kwani tunafanya uchechemuzi ili wananchi wapate taarifa zinazowaletea maendeleo."


Nae Salim Said Salim, mwandishi wa habari mwandamizi Zanzibar aliwahimiza waandishi wa habari kuzungumzia kifungu baada ya kifungu badala ya kuangalia mapungufu ya sheria kwa ujumla ili kusaidia kufanikisha lengo la uchechemzi wa mabadiliko ya sheria hizo.


“sisi waandishi wa habari tunao wajibu mkubwa wa kuwafahamisha viongozi na wananchi wote kwamba tunapozungumzia uhuru wa habari si kwa manufaa ya waandishi na vyombo vya habari tu bali ni kwa manufaa ya jamii nzima kupata huduma zao muhimu,” Salim Said Salim, mwandishi wa habari mwandamizi Zanzibar.
 

Mwandishi wa habari mwandamizi Zanzibar, Salim Said Salim akifafanua jambo

Wakichangia mada katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, kanda ya Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Internews Tanzania walisema sheria zinazosimamia vyombo vya habari Zanzibar zinahitaji kufanyiwa marekebisho kutokana na baadhi ya vifungu vya sheria hizo kukandamiza uhuru wa habari.


Walitaja miongoni mwa sheria ambazo zimebainika kuwa na mapungufu yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ni sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria Na.8 ya mwaka 1997, sheria ya Tume ya Utangazaji ya Zanzibar Na. 7 ya mwaka 1997 kama ilivyorekebishwa na sheria namba 1 ya mwaka 2010 pamoja na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.

Nyingine ni sheria ya kufuta sheria ya Baraza la Wawakilishi (kinga, uwezo na fursa) namba. 4 ya 2007 na kutunga sheria mpya ya Baraza la Wawakilishi (kinga, uwezo na fursa) katika  kutekeleza kazi na mambo mengine yanayohusiana na hayo Na. 6 ya 2022, Sheria ya kufuta Sheria ya Uchaguzi namba. 11 ya 1984 na kutunga sheria ya uchaguzi ya mwaka 2017 na masuala mengine yanayohusiana nayo pamoja na sheria ya kufuta sheria ya adhabu Na. 6 ya 2004 na kutunga sheria mpya ya adhabu, kuweka masharti bora zaidi pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo.


"kukiwa na sheria zinazotoa fursa kwa vyombo vya habari kutekeleza wajibu wake kwa uhuru bila vikwazo vya kisheria kunatoa nafasi kwa waandishi wa habari kusaidia jamii na mamlaka kuibua changamoto zilizopo katika maeneo mbalimbali na kutatuliwa kwa wakati" alisema


Mwandishi kutoka Zenj Tv Berema Suleiman Nassor, mwandishi wa habari kutoka Zenji FM alisema sheria kutoweka haki ya mwandishi wa habari kupata taarifa kutoka kwa mamlaka mbalimbali kunayima haki waandishi wa habari kupata baadhi ya taarifa pale zinapohitajika.  


Alisema “unaweza kwenda kwenye ofisi kutaka taarifa fulani lakini kiongozi akakuzungusha na kukunyima kabisa taarifa kwasababu anajua hakuna sheria inayomlazimisha kutoa tarifa kwa mwandishi, tunaomba hiki kifungu kiwekwe kwenye sheria kwani tunakumbana na changamoto pale tunapokuwa tunahitaji kupata taarifa kutoka sehemu Fulani.”  


TAMWA Zanzibar, shirika la Internews Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari Zanzibar wanaendelea kuangalia mapungufu yaliyopo katika sheria zinazosimamia sekta ya habari Zanzibar ili ziweze kufanyiwa marekibisho kwa lengo la kuweka mazingira rafiki ya vyombo vya habari Zanzibar kutekeleza majukumu yake kwa uhuru.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...