Skip to main content

"Usawa wa Kijinsia kwenye Michezo ni chachu ya Mabadiliko kwenye Jamii" Bi. Hawra Shamte

Na, Hassan Msellem, Pemba



Mwandishi mwandamizi Zanzibar Bi. Hawra Shamte, amesema katika miaka ya hivi karibuni michezo imedhihirisha uwezo wake mkubwa wa kuendeleza uwezeshaji wa Wanawake na wasichana, hivyo jamii inapaswa kubadili mitazamo hasi juu ya suala la michezo kwa Wanawake ili nao waweze kupata haki yao ya msingi ya kushiriki katika Michezo.


Ameongeza kuwa michezo huchukuliwa kuwa ni haki ya wanaume pekee ambapo dhana hiyo hupelekea wavulana kutilia maanani zaidi suala la michezo na wasichana wakijikuta wanaachwa nyuma na kupelekea kutokuwepo kwa usawa wa Kijinsia kwenye michezo.


Sambamba na hilo amesema michezo inahamasisha kuzungumza na Vijana na kuunganisha vizazi kijamii na kiutamaduni, hivyo Waandishi wa Habari na wadau wa michezo wana jukumu la kuihamaisha jamii kuwa na mitazamo mizuri juu ya usawa wa Kijinsia katika Michezo.


"Linapokuja suala michezo kuanzia ngazi ya jamii Hadi taifa linaonekana ni jambo linalowahusu wavulana peke yake, kiasi kwamba wasichana wamejikuta wao hawahusiki kabisa kwenye michezo Hali hii inapelekea usawa wa Kijinsia kwenye michezo kubaki kuwa ndoto tu, hivyo ni wajibu wenu Waandishi wa Habari kuanza kuandika habari zinashajihisha na kuonesha umuhimu wa usawa Kijinsia kwenye michezo katika jamii zetu" alisema


Alisema licha ya wavulana kuona wao ndio pekee Wana haki ya kushiriki katika Michezo bado Kuna tatizo la unyanyapaaji wa Kijinsia kwani wanaume ambao wanaonekana kutokuwa na uwezo mzuri wa kushiriki kwenye michezo hubaguliwa na wanaume wenzao na kujiona wamekosa dhaifu na wamekosa thamani jambo ambalo hupelekea baadhi yao kujiingiza kwenye vitendo viovu ikiwemo vya utumiaji wa dawa za kulevya na kushiriki mapenzi ya jinsia moja.


Alisema "Hii dhana potofu haiwaathiri wasichana tu, Bali hata wavulana ambao walitegemewa kuwa wakakamavu, wavulana ambao hawana uwezo wa ukakamavu wa kimwili au Wana michezo wazuri hupata dhihaka na aibu kulingana na itikadi Kali ya kiume inayojumuisha nguvu, misuli, ukosefu wa huruma" 


Amenena hayo katika Ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania Mkanjuni Pemba katika mafunzo ya siku tano kwa Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba, katika mradi wa mwaka mmoja katika kukuza usawa wa Kijinsia katika Michezo (Cohort Gender and Sports) ambao umeanza Mwezi March 2024 na kutarajiwa kukamilika February 2025.




Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...