Skip to main content

Tutasubiri upatikanaji wa sheria mpya za Habari Zanzibar mpaka lini? - Wadau

 ADAU wa vyombo vya habari wameiomba serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukamilisha mchakato wa marekebisho ya sheria za habari zilizotolewa maoni na wadau ili  kutoa mazingira rafiki kwa waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao bila vikwazo.

 

Imeelezwa kwa muda mrefu licha ya wadau mbalimbali kutoa na kuwasilisha mapendekezo yao kuhusu mapungufu yaliyopo kwenye baadhi ya sheria hizo, lakini utekelezaji wake bado umekuwa wa kusuasua jambo linalopelekea mazingira magumu ya utendaji kazi wa vyombo vya habari nchini.

 


Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dkt. Mzuri Issa alieleza mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari umekuwepo kwa miaka mingi lakini bado sheria hizo ambazo nyingi ni za muda mrefu zimekwama kurekebishwa.

 

"Sisi wengine tangu tuko waandishi chipukizi tunazungumzia kupata hizi sheria mpya za habari, tangu 2008 kwa kweli ni muda mrefu, tunahitaji kusimamia jambo hili kwa umoja wetu na hatimae tupate sheria mpya za habari Zanzibar," alieleza Dkt. Mzuri katika kongamano hilo.

 

Aliongeza wadau wa habari wamefanya mapitio ya sheria nane za habari ikiwemo Sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria no.8 ya 1997, Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar namba 7 ya mwaka 1997  iliyorekebishwa na sheria namba 1 ya mwaka 2010 na kuwasilisha ripoti ya mapendekezo yao kwa mamlaka husika ikiwemo kukutana na Rais na waziri.

 

Aliongeza kuwa "tumewahi kuzungumza na Mhe. Rais kuhusu sheria hizi na Waziri pia, nadhani inabidi tupange kuzungumza nao tena ili tuone hili linakwendaje. Haitapendeza hata kidogo tumalize mwaka huu na bado hatujapata mabadiliko ya sheria za habari.”

 

Akigusia kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na mabadiliko ya tabianchi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura, alieleza vyombo vya habari vitatekeleza kwa ufanisi wajibu wao katika kulinda mazingira iwapo waandishi watakuwa huru kupata na kutoa taarifa bila hofu kisheria.

 

Alieleza, “kaulimbiu ya kimataifa mwaka huu ilijikita katika uhifadhi wa mazingira. Lakini kwakweli bila kuwa na sheria nzuri za habari hatuwezi kutekeleza hayo tunayoyataka. Waandishi wa habari tunahitaji uhuru wa kupata taarifa ili tuweze kutekeleza uandishi wa habari mahususi. Hatuwezi kuyatekeleza hayo kama sheria hazitutengenezei mazingira ya kulinda uhuru wetu.”

 

Katika hatua nyingine alivitaka vyombo vya habari kubuni mbinu mpya za kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kufikiria namna ya kuendana na kasi ya mageuzi ya masuala ya kiteknolojia ili kulinda uhuru wao.

 

"Sahizi changamoto kubwa inayoathiri uhuru wa habari ni masuala ya kiuchumi katika vyombo vya habari. Tunaitaji kuangalia upenyo ili kuona namna gani kile kinachosababisha madhara katika vyombo vya habari kinatatuliwa," alibainisha katibu mtendaji huyo.

 

Akifafanua kuhusu maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari Zanzibar, Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji, Suleiman Salim alieleza tayari mapendekezo ya sheria hizo yapo ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kwaajili ya hatua zaidi.

 

"Kwa sasa mswada wa sheria ya habari ipo kwa mwanasheria mkuu, na tunaitegemea itakwenda baraza la wawakilishi kama mswada na tunawaomba walioko kule waichangie vizuri ili iweze kupita na tupate sheria mpya," Suleiman Salim, Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji aliwaambia wadau.


Aidha Suleiman alisema tayari serikali imekamilisha mchakato wa kuandaa Sera mpya ya habari Zanzibar na kuwatoa hofu wadau wa habari juu ya uwepo wa sera hiyo kuwa itazinduliwa muda sio mrefu.

 

Akichangia mdahalo kwenye maadhimisho hayo, Salim Said ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe alieleza uwepo wa sheria bora ni muhimu katika kuwezesha mazingira bora ya waandishi wa habari kuwajibika.

 

"Vyombo vya habari ni washirika wa maendeleo, hivyo kuwa na sera na sheria bora itawawezesha waandishi wa habari kuwa na mazingira rafiki katika  kutekeleza majukumu yao," alifahamisha, mwandishi wa habari huyo mkongwe Zanzibar.

 

Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari 2024 yameandaliwa Baraza la habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar (MCT ZNZ), Chama cha Waandshi wa Habari Tanzania Zanzibar (TAMWA,ZNZ) Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA), Klabu ya Waandishi wa Wabari Zanzibar (ZPC) na Shirika la Commonwealth Foundation yakiambatana na kaulimbiu ya  “UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NA MAGEUZI YA SERA NA SHERIA ZA  HABARI ZANZIBAR. ”



Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...