Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba likusanya Shillingi laki saba na eflu tisini na tano kutokana na faini za makosa ya usalama barabarani.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limekusanya Shillingi laki Saba na elfu tisini na tano kutoka tarehe 24\02\2022 hadi March 02\2022 kutokana na operesheni ya ukaguzi wa vyombo vya maringi mawili na Matatu yani Pikipiki na Bajaji ambapo Kwa kipindi hicho takriban vyombo 105 vilikamatwa Kwa makosa mbali mbali ikiwemo Madereva kutokuwa na leseni, uzembe, vyombo kukosa pasi nakadhalika ambapo Madereva 60 walifikishwa mahakamani na kutozwa faini.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Kamishna msaidizi wa Polisi Richard Tadeo Mchomvu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Madungu Chake Chake.
Aidha Kamanda Richard ametoa wito waendeshaji wa vyombo vya Moto hususan madereva Bodaboda kuwa Makini na kufuata Sheria za Usalama Barabarani ili kuepukana na Ajali zisizo za lazima.
Comments
Post a Comment