Skip to main content

Uzembe wa madereva wasababisha vifo vya watu 2 katika ajali mbili tofauti Pemba.

 Habari Na, Hassan Msellem-Pemba.


Hassan Ali Hassan miaka 20, amefariki dunia baada ya gari aliokuwa amepanda aina ya Hino Lorry yenye namba ya usajili Z 572 ES iliokuwa ikiendeshwa na Ali Juma Hassan miaka 35, mkaazi wa Vitongoji kupata ajali katika eneo la Meli tano Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Akizungumza na Bahari fm Radio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Richard Mchomvu, alisema majira ya saa 8 mchana wakati gari hiyo ikitokea maeneo ya Ole kuelekea Ziwani ikiwa imebeba watu sita (6) ilipofika eneo la Meli Tano kutokana na mwendo kasi iliacha njia na kuelekea mabondeni kitendo kilichopelekea mtu mmoja kufariki dunia papo hapo na wengine wa tano kujeruhiwa.

Aidha Kamanda Mchomvu aliwataja majeruhi hao kuwa ni Iddi Omar Mgunya mwenye umri wa miaka 35, mkaazi wa Vitongoji, Said Ali Said miaka 25, mshirazi wa Vitongoji, Khamis Ali Shaaban miaka 19 mkaazi wa Vitongoji, Nassor Said Khamis miaka15 mkaazi wa Vitongoji ambapo wamelekwa hospitali kwa ajili matibabu zaidi na afya zao zinaendelea vizuri.

Katika ajali nyengine kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ayoub Hamad miaka 22, mkaazi wa Kwale Kisiwani Pemba amepoteza maisha baada ya gari alilokuwa amepanda kupata ajali eneo la Mtuhaliwa baada ya dereva wa gari hiyo ku-over take na kupelekea kugongana uso kwa uso na gari aina ya Carry jambo lililopelekea kijana huyo kupata majeraha maeneo ya kichgwani na kupelekea kupoteza maisha papo hapo.

Akisimulia kuhusu ajali hiyo Kamanda Mchomvu amesema gari hiyo ya abiria yenye namba ya usajili Z105 BL iliokuwa ikitokea Chake Chake kuelekea Mkoani alipofika maeneo ya Mtuhaliwa ili over take msafara wa gari zinazokwenda harusini na kusababisha kutokea kwa ajali hiyo.

Waliopata majeraha katika ajali hiyo ni Suleimana Nassor Shaib 23 mshirazi wa Chake Chake, Said Ali 25 mshirazi wa Ndagoni, Abas Issa 17, mshirazi wa Chake Chake, Hamad Seif 51 na Omar Ali 40 Msingini, amesema majeruhi wote wamefikishwa katika hospitali ya Abdalla Mzee kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


"Ni kweli jana majira ya saa 2 asubuhi kijana hassan Ali Hassan miaka 20, amefariki dunia baada ya gari aliokuwa amepanda aina ya Hino Lorry yenye namba ya usajili Z 572 ES iliokuwa ikiendeshwa na Ali Juma Hassan miaka 35, mkaazi wa Vitongoji kupata ajali katika eneo la Meli tano Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba" alisema

Amesema ajali zote mbili zimesababishwa na uzembe wa madereva kwakutozingatia sheria ya usalama barabarani, hivyo basi amewaomba madereva kuwa makini pindi wanapokuwa barabarani na amesema endapo atatokea na dereva yeyote atakaevunja sheria za usalama barabarani hatua kali za kisheria zitakuchukuliwa dhidi yake ikiwemo kunyan’ganywa leseni.

Habari hii niliichapisha kwenye ukurasa wangu wa Facebook August 20, 2021 kwa ushahidi wa kiungo (link) hichi kabla ya kuanzisha blog ya Pemba Post Blog ambayo nimeichapisha habari hii.

Link of Facebook above👇

https://www.facebook.com/share/p/fvjr29RatJGi44LA/?mibextid=oFDknk

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

The carelessness of drivers caused the death of 2 people in two separate accidents in Pemba.

Written By, Hassan Msellem-Pemba.


A person known as Hassan Ali Hassan 20, died after the car he was riding in, a Hino Lorry with registration number Z 572 ES, which was driven by Ali Juma Hassan 35, a resident of Vitongoji, after having an accident in Meli tano area.


Speaking to Bahari fm Radio, South Pemba Regional Police Commander Richard Mchomvu said that at around 8 o'clock in the afternoon when the car was coming from Ole area towards Zwani carrying six (6) people, when it reached Meli five area due to high speed, it left the road and headed towards in the valleys, an act that led to the death of one person on the spot and the injury of five others.


In addition, Commander Mchomvu named the injured as Iddi Omar Mgunya, 35, a resident of Vitongoji, Said Ali Said, 25, resident of Vitongoji, Khamis Ali Shaaban, 19, a resident of Vitongoji, Nassor Said Khamis, 15, a resident of Vitongoji, where they were taken to hospital for further treatment and health they are doing well.


In another accident, a young man known as Ayoub Hamad, 22, a resident of Kwale Kisiwani Pemba, lost his life after the car he was riding in met with an accident in Mtuhaliwa area after the driver of the car went overboard and collided head-on with a Carry car. which led to the young man getting injuries in the groin areas and leading to the loss of life on the spot.


Speaking about the accident, Commander Mchomvu said that the passenger car with registration number Z105 BL was coming from Chake Chake towards the Region when he arrived at Mtuhaliwa to take over the convoy of cars going to the wedding and caused the accident.


Suleimana Nassor Shaib, 23, from Chake Chake, Said Ali, 25, from Ndagoni, Abas Issa, 17, from Chake Chake, Hamad Seif, 51, and Omar Ali, 40, were injured in the accident. for treatment.


He said that both accidents were caused by the negligence of the drivers for not following the road safety law, so he asked the drivers to be careful when they are on the road and he said that if he happens to any driver who breaks the road safety laws, strict legal measures will be taken against him, including the confiscation of his license.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...