Skip to main content

"Zingatieni maadili na ufanisi wa kazi zenu ili kuandika habari zenye ubora zaidi" RC Kusini Pemba

Habari Na, Hassan Msellem, Pemba.


Waandishi Kisiwani Pemba watakiwa kufuata maadili ya kazi zao, ili kuepuka kuingia kwenye makosa pamoja na kuandika habari zitakazoweza kutoa mchango kwa taifa.



Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari, leo Mei 18, 2024 uliofanyika ukumbi wa Chuo cha Samail Gombani Chake chake Pemba, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, alisema Waandishi ni sauti ya wasio na sauti hivyo wanapaswa kuandika habari ambazo zitaweza kuwasaidia Wananchi.


Aidha amewataka Waandishi hao kufuata maadili na ufanisi katika kazi zao Ili kuepukana na makosa mbali mbali pamoja na kuandika habari zenye kuleta mabadiliko chanya katika Umma.


"Siku hii ya uhuru wa habari ni muhimu kujitafakari kwamba tunafanya kazi kwa kiasi gani, tuna uhuru kiasi gani, vikwazo gani tunavyopitia na kupanga mikakati ya kuweza kutatua," alisema Mkuu huyo. 


Mkuu huyo aliwataka waandishi hao kuibua changamoto za wananchi na kuzisemea, ili ziweze kupatiwa ufumbuzi, kwani sauti ya mwandishi ndio inayosaidia katika kuleta mabadiliko na maendeleo katika nchi. 


Aidha aliwataka waandishi kuelimisha jamii juu ya kuhifadhi mazingira, ili yawe safi na kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa yakiathiri maisha ya wananchi. 


Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau, aliwasisitiza Waandishi hao kuwa na kadi maalumu zinavyotolewa na idara ya Habari maelezo Ili kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi sambamba na kuwataka Waandishi wanaomiliki runinga za mtandaoni kuvisajili vyombo vyao Ili viweze kutambuliwa na kufanya kazi kwa kufuata maadili ya Habari.


"Niwaombe waandishi wote wawe na vitambulisho maalumu vinavyotolewa na idara ya Habari maelezo Ili muwe huru katika utekelezaji wa majukumu yenu napia niwaombe wale wote wenye online TV na blogi wajisajili na kutafuta kadi ya uandishi, kwani kuna baadhi ya watu wanatumia mwamvuli wa waandishi kujifanya mwandishi na kuleta taharuki kwa Umma," alisema Mdhamini huyo. 


"Tena inasikitisha sana kuona baadhi ya viongozi wa chama na Serikali wanatafuta watu ambao hawana taaluma ya habari na kuwatumia kama Wana habari mbona hawajifanyi madaktari, askari au wanajeshi kwanini mtu ajifanye mwandishi wa Habari haliyakuwa hana taaluma ya habari kwakweli nachukizwa sana na hii tabia na naahidi Mimi kama afisa mwenye jukumu la kusimamia tasnia ya Habari Kisiwani Pemba nitahakikisha nawachukulia hatua za kisheria wale wote ambao wanajifanya Waandishi wa Habari ambao hawana taaluma ya habari" alisema


Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC) Bakar Mussa Juma, alisema waandishi wa habari katika Klabu hiyo wanafanya kazi vizuri na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, hivyo ameiomba jamii na viongozi mbali mbali kuendelea kuwapa ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu ya kazi zao kwa uhuru na ufanisi zaidi.


Aliongeza kuwa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba ina malengo ya kuanzisha Radio na television ili kutoa fursa kwa Waandishi wa Habari kufanya kazi zao ambapo kwa sasa wameanza na blogi ambayo imeanza kutoa mafanikio makubwa kwa Klabu hiyo.


Akiwasilisha mada katika maadhimisho hayo mwandishi wa habari na Mjumbe kutoka PPC Bwana Gasper Charles,  alisema waandishi wa habari wana jukumu la kulinda na kuelimisha jamii kuhifadhi mazingira ambayo yanayopelekea athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi ambayo yamekuwa ni tatizo linalopaswa kupigiwa kelele mara kwa mara.


Maadhimisho hayo ya siku ya uhuru wa habari yamefanyika katika Ukumbi wa Samael Gombani Chake Chake ambayo yameandaliwa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC) kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...