AJISALIMISHA KITUO CHA POLISI KUDAI MTOTO WAKE ALIYEMTUPA. Novemba 15.2025 kipindi Cha Mawio kiliripoti tukio la mtoto mchanga wakike mweye umri wa wiki moja kutupwa huko Kitope ambapo aliyemtupa mtoto hakufahamika Hatimae Jana Novemba 21.2025 Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Tattu Mohamed mwenye umri wa miaka 26, mkaazi wa Mfenesini Unguja, Zanzibar amejisalimisha katika Kituo cha Polisi Mahonda kudai mtoto wake na kusema sababu zilizopelekea kumtupa mtoto wake ni tatizo la kupatwa na mashetani. Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Benedict Mapujila, amesema Mama huyo alikwenda kujisalimisha Kituo Cha Polisi Mahonda na kukiri kuwa yeye ndiye aliyemtupa mtoto huyo kutokana na kupatwa na matatizo ya mashetani ambaye ni mtoto wake Tatu ingawa alimzaa nje ya ndoa. Aidha Kamanda Mapujila, amesema kumtupa mtoto ni Kosa Kisheria hivyo Jeshi la Polisi litamshtaki Mama ili Sheria ifate mkondo wake na kutoa wito kwa jamii kutokufanya maamuzi ambayo yako kinyu...