Taarifa na Mwandishi Wetu.
Inadaiwa taarifa za kichanga hicho kufariki dunia zilisambaa jana April 28, 2024 baada ya mama anayefahamika kwa jina la Saumu Hamduni Juma Mkaazi wa Michungwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, kujifungua watoto mapacha akiwa na ujauzito wa miezi sita katika hospitali ya Chake Chake na kusababisha hali za vichanga hivyo kuhitaji huduma ya dharura ya oksijini, ambayo ilikosekana katika hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa Afisa Ustawi wa Wilaya ya Chake Chake, Afisa Ustawi wa Wilaya, Afisa Afya wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Haji Ali na Daktari Dhama wa Wilaya ya Chake Chake (DMO) Sharif Hamad Khatib ambao walinukuliwa na afisa watu wenye ulemavu Wilaya ya Chake Chake Mwadini Juma Ali alisema
“Nikweli jana majira ya mchana alifikishwa mama mjamzito katika Hospital ya Chake Chake na hatimaye kujifungua watoto wawili pacha ila mama huyo alijifungua akiwa bado muda wa kujifungua kitaalamu kufika ambapo ni miezi saba na hatimaye kujifungua akiwa na miezi saba” wakati wa kujifungua mtoto mmoja alifariki na yule mwengine alikuwa anahitaji Oksijini kwa wakati ule kwa mujibu wa daktari aliyetoa huduma ila tatizo likaja mashine ya Oksijini hakuwepo kwa wakati ule na alikuwa iko Hospital ya Vitongoji kwenye gari ya kubebea wagonjwa ikiwa iko njiani kutoka Mkoani na baada ya kufika kwa mashine hiyo mtoto alipatiwa huduma na mpaka sasa yuko Hospitali ya Chake Chake anaendelea vizuri Alhamdullilah”
Kwa mujibu wa taarifa hii inamaanisha
taarifa zilizotolewa awali ambazo zilisema kifo cha kichanga hicho kilitokana
na kukosekana kwa gari ya kubebea wagonjwa (ambulensi) katika
hospitali hiyo hazikuwa taarifa sahihi.
%20-%20Copy.jpeg)
Comments
Post a Comment