Makala Na Fatma M. Suleiman, Unguja “Sijatokea kwenye familia yenye uzoefu wa kisiasa, nimepata hamasa kuionyesha jamii mwanamke anaweza kuwa kiongozi na kutatua changamoto za jamii Mwanamke ni mlezi, mbunifu na mwenye fikra pevu, kwa hiyo hakuna sababu ya kunizuia kuingia kwenye uongozi wa kisiasa.” Kauli hii inaakisi Taarifa ya Baraza la Taifa la Wanawake, Tanzania, 2023 inayoeleza kwamba “Kuhakikisha usawa wa kijinsia katika uongozi si chaguo, bali ni wajibu wa kijamii.” Rahima Said Abdallah ni mfano wa mwanamke jasiri aliyevunja vikwazo vya kijamii na kugombea nafasi ya uwakilishi kupitia Chama cha Ukombozi wa umma (CHAUMMA) Jimbo la Mwanakwerekwe katika Uchaguzi Mkuu wa 2025. Rahima ana miaka 26 amethibitisha kuwa uongozi haujali jinsia, bali ni uwezo, bidii na dhamira ya kweli ya kuwatumikia watu. Kupitia safari yake, amekuwa kielelezo cha matumaini mapya kwa wanawake na vijana wanaotamani kushiriki katika uongozi wa kisiasa nchini. Rahima alizaliwa mwaka 1...