Na, Hassan Msellem, Pemba
Walimu wa Skuli ya msingi Michakaini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, wameiomba Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar kuandaa bajeti maalumu kwenda maskulini Ili kusaidia Klabu za Michezo.
Wakizungumza na mwandishi wa Habari hizi, Mwalimu wa somo la michezo Habiba Juma Jafar na Mwalimu Subira Abdalla Saleh, walisema kutokana changamoto za ukosefu wa fedha na mazingira rafiki ya kufanyia michezo inawalazimu katika mashindano ya elimu ya malipo pekee jambo linalochangia kurudisha nyuma harakati za michezo skulini hapo.
"Hapa Skuli tunaprogramu za michezo mbali mbali ikiwemo michezo ya mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa wavu, kuimba utenzi, ngonjera, mbio za magunia nakadhalika lakini ukiangalia tunashindwa kuendeleza michezo hii kwasababu tunakosa bajeti za mazingira rafiki ya kuendeleza maana hapa Skuli hakuna mazingira ya Uwanja ya kushiriki michezo yote hiyo"
Alieleza faida ya kushiriki katika mchezo kwa wanafunzi hususan kwa wasichana mwalimu wa somo la afya na michezo katika Skuli hiyo Fatma Haji Ali, alisema michezo Ina faida nyingi kiafya ikiwemo kuepukana na maradhi mbali mbali na udumavu wa akili pamoja na kuongeza ufahamu kwa wanafunzi.
"Kwakweli Kuna faida nyingi sana kwa wanafunzi kushiriki katika Michezo miongoni mwa faida hizo zipo za kiafya lakini pia za kimaisha kwa upande wa afya mwanafunzi anayeshiriki michezo anakuwa na afya imara kwani anapata ushangamfu wa kimwili, kiakili, ufahamu pia unaongezeka lakini inaweza kumpa ajira pindi akimaliza masomo"
Nasra Juma Rajab ni mwanafunzi wa darasa la tano anayeshiriki michezo wa mpira wa kikapu na nage alisema michezo imewezesha kuwa na afya mzuri, uchangamfu pamoja na kuongeza ufahamu katika masomo.
"Napenda sana michezo kwasababu napata kuchangamka, afya mzuri lakini hata ufahamu wangu unakuwa mzuri, naomba uongozi wa Skuli uendelee kuimarisha michezo ili tuzidi kufika mbali kimichezo hususan michezo tunayoweza kushiriki wanafunzi wakike ikiwemo mchezo wa netball, kuimba, kusoma utenzi na nage"
Arkam Abdi Hamza, ni mwanafunzi wa darasa na mchezi nguli wa mpira wa miguu katika Skuli ya msingi Michakaini, amewaomba wanafunzi wenzake kushiriki katika michezo inayochezwa skulini hapo Ili waweze kunufaika na faida za michezo ikiwemo kuwa na afya imara ya kimwili na kiakili pamoja kupata zawadi mbali mbali ikiwemo madaftari, viatu, sare pamoja na Fedha.
"Nawaomba wanafunzi wenzangu wapende michezo kama ninavyopenda Mimi kwani kupitia michezo nimepata faida nyingi nimewahi kupewa viatu, madaftari, mkoba na pesa kupitia mashindano ya elimu bila ya malipo yaliyomalizika hivi karibuni"






Comments
Post a Comment