Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Current News

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...

WANACHAMA 25 WA VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA KUSINI UNGUJA WANOLEWA KIBIASHARA.

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA  Jumla ya wanachama 25 kutoka vikundi 16 vya kuweka na kukopa katika Wilaya ya Kusini Unguja wamepatiwa mafunzo ya siku mbili ya kuchagua, kupanga na kusimamia biashara, chini ya Programu ya Mashirikiano ya Pamoja kwa ajili ya Haki za Watu wenye Ulemavu (CADiR) inayotekelezwa na Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Shirikisho la Jumuiya za Watu wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) na Jumuiya ya wasioona Zanzibar (ZANAB) kwa ushirikiano mkubwa na Shirika la Watu Wenye Ulemavu la Norway (NAD). Washiriki hao ambao 16 ni watu wenye ulemavu na 9 ni walezi na wasimamizi wa Watoto wenye ulemavu wamehudhuria mafunzo kama wawakilishi wa vikundi vyao, na wanatarajiwa kuyafikisha maarifa haya kwa wanachama wenzao, ili kila kikundi kinufaike kwa pamoja na kuimarisha biashara zake. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Aziza Ismail ambae ni Mratibu wa program ya CADiR kutoka NAD, amesema taasisi zinazoshirikiana katika programu...

VIONGOZI WA 'ACT' KIZUIZINI UWANJA WA NDEGE ANGOLA

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman na Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu wanadaiwa kuzuiwa kuingia nchini Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD).  Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwenye msafara wake ameambatana na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Nasra Nassor Omar na maofisa wengine wa chama hicho. Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo-Zanzibar, Ismail Jussa ameliambia Mwananchi leo Alhamisi Machi 13, 2025 kuwa Othman na msafara wake wamezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Luanda jijini Angola.   Tayari ACT Wazalendo imetoa taarifa ya kulaani tukio hilo ililoliita la udhalilishaji wa kiongozi huyo huku kamati yake ya uongozi ikikutana kwa dharura kujadili suala hilo, ambalo mamlaka za Angola hazijajitokeza kulizungumzia. Wakati huohuo, Lissu ameandika kwenye ukurasa wake wa X kuwa mamlaka za uhamiaji za Angola zimewazuia na kukataa kuwaruh...

MAREKANI KUFUTA ASILIMIA 80 YA PROGRAMU ZINAZOFADHILIWA NA USAID.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya programu zinazofadhiliwa na Shirika la Marekani la Misaada ya Kimataifa (USAID) zitafutwa. #AzamTVUpdates Mhariri | John Mbalamwezi

JESHI LA POLISI LAENDELEA KUMSHIKILIA MWAKINYO

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa sababu ya kuendelea kumshikilia bondia maarufu nchini Hassan Mwakinyo (29), anayetuhumiwa kumshambulia mkazi wa jijini Tanga Mussa Ally akimtuhumu kuwa ni mwizi. Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jumatatu Machi 10, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema Mwakinyo anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi Mussa Ally ambae anadai ni mvuvi alipopita kwenye makazi yake huku akibainisha kuwa uchunguzi utakapokamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya habari ikiwa ni sambamba na kumfikisha mahakamani ili ajibu tuhuma zitakazomkabili.  Kamanda Mchunguzi amesemna wamemkamata Mwakinyo kwa tuhuma za kumjeruhi mvuvi, ambapo ni tuhuma za jinai huku akifafanua kuwa mtu yeyote akifanya makosa kama hayo bila kuangalia nafasi yake kwenye jamii, anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na suala la umaarufu haliwezi kubadili kile kilichotendeka. “Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia Hassan Mwakinyo (29) mkazi wa Sahare...

ALIYEBUNI JINA 'TANZANIA' AFARIKI DUNIA

Aliyebuni jina la taifa la Tanzania, Mohanmmed Iqbal Dar, amefariki Dunia akiwa usingizini jijini Birmingham, Uingereza alikokuwa akiishi akiwa na umri wa miaka 80. Mohammed Iqbal Dar aliyezaliwa Agosti 8, 1944, mjini Tanga, alikuwa mtoto wa Dk Tufail Ahmad Dar, daktari maarufu aliyehudumu katika mikoa ya Tanga na Morogoro nchini Tanzania. Mwaka 1965 alihamia Uingereza alipokuwa akiishi hadi kifo chake. Igbal alishiriki katika shindano la kutafuta jina la Tanzania lililoandaliwa mwaka 1964 kabla ya Muungano ambako yeye alikuwa mmoja wa wanafunzi 80 walioshindana na hatimaye yeye kuibuka mshindi. Akizungumzia jinsi alivyobuni jina TANZANIA enzi za uhai wake Iqbal alisema alichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar nikachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha nikaunganisha nikapata jina TANZAN. Baada ya hapo alichukua herufi ya kwanza ya jina lake ‘lqbal’ kisha akachukua herufi ya kwanza A ya jina la dini yake yaani Ahmadiya na kuunda jina ...

MWANAFUNZI 'SUA' AFARIKI KWA KUJINYONGA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linachunguza tukio la kifo cha Yosia Johani Keya (25) mwanachuo wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA), aliyekutwa amejinyonga kwa kutumia shuka ambalo alilifunga kwenye kenchi la makazi ya wanachuo upande wa baraza la nyuma. Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama, imeeleza kuwa tukio hilo limefahamika leo Machi 9, 2025 asubuhi katika eneo la makaazi ya wanachuo hao kampasi ya Mazimbu, kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro.  "Marehemu amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia shuka ambalo alifunga kwenye Kenchi la makazi ya wanachuo upande wa baraza la nyuma, uchunguzi wa tukio hilo umeanza ili kubaini chanzo cha tukio hilo. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa vijana na watu wengine kuacha kuchukua maamuzi kama hayo ya kujitoa uhai kama suluhu ya changamoto zao, badala yake watumie fursa ya madawati mbalimbali ya ushauri nasaha na nasihi kueleza changamoto hizo," imeeleza taarifa hiyo  Chanzo; EastAfricaTV ...

"UCHUMI WA BULUU NI BIASHARA KATI YA SERIKALI NA BENKI YA CRDB CRDB" MWENYEKITI WA ADC TAIFA-SHABANI ITUTU.

Na, Hassan Msellem, Pemba  M wenyekiti wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Taifa Shabani Itutu, ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu kuboresha hali za Wananchi kupitia Sera ya Uchumi wa Buluu, ambayo mpaka sasa haijafikiwa ipaswavyo. Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wanachama wa wa Chama cha ADC na Wananchi mbali mbali Kisiwani Pemba, amesema licha ya Serikali ya awamu ya nane kuanzisha Sera ya Uchumi wa Buluu kwa lengo la Kuboresha Hali za Wananchi kupitia rasilimali za baharini ikiwemo uvuvi wa Samaki na zao la mwani bado hali za Wananchi kupitia rasilimali hizo hazijaimarika. Akitaja sababu zinazobabisha kutokufikiwa kwa Sera ya Uchumi wa buluu kwa Wananchi ni pamoja kukosekana kwa vyombo vya kisasa vya uvuvi, kukosekana kwa viwanda vya kusindika samaki pamoja kutokufanya kazi kwa viwanda vya kuchakata zao la mwani. "Tunaamini dhamira ya Serikali ni njema sana kupitia Sera ya Uchumi...

Wananchi waiomba Serikali kuweka vizuwizi barabara ya Pagali kueousha ajali.

 S alim Hamad,Pemba Wananchi wa Shehia ya Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba,wameiyomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuifanyia maboresho njia ya kutoka Ikulu ya Pagali kueleke Pondeani na Wesha kutokana na kusababisha ajali za mara kwa mara. Wananchi hao wametoa kauli hiyo mara baada ya gari aina Ton hais kuacha njia na kuingia kwenye msingi ingawa hakuna aliyemajuri wala kupoteza maisha. Msabah Said Mkaazi wa Tibirinzi amesema Njia hiyo ambayo haipiti mwezi imekuwa ikisababisha ajili kutokana na kuwepo kwa kibonde wakati wakuteremsha mlima huo. Amesema mara nyingi gari au vyombo vya maringi mawili ndio vinaaongoza kwa kupata ajali kwa vile baada kushuka zinafeli breki na hatimai kuingia misingi jambo ambalo linaweza kuja kuleta maafa makubwa zaidi kama Serikali haikuchukua hatua. ‘’Tunaomba Seikali hii njia ya kutoka Ikulu Pagali kuifanyia marekebisha mana mlima ni mkubwa na huku chini kumefanya kibonde sasa wakati gari zikipta anataka kupinda kuelekea wesha mara ny...

Waandishi wa habari chipukizi wapongezwa kwa kutendea haki mradi wa SWIL.

Na, Thuwaiba Habibu. Mwenyekiti wa kamati ya utetezi kutoka Tamwa Bi shifaa said hassani amewapongeza waandishi wa habari chipukizi kutendea haki mradi wa wanawake na uongozi kwa kufanya kazi kwa kitaalamu zaidi. Ameyasema hayo katika sherehe ya mahafali ya waandishi wa habari chipukizi yaliofanyika ukumbi wa bima mpira mkabala na kituo cha polisi madema alisema hawa waandishi wa habari chipukizi wameweza kutendea haki mradi wa wanawake na uongozi na kuweza kuibua vitu ambavyo walivisahau kama vipo katika jamii yao na kuweza kuviandikia makala za magazeti vipindi vya Redio na TV. Alisema tumezoweya kuona makala zinazomuhusu mtu anahojiwa mtu mmoja peke yake lakini wao walitumia vyanzo tofauti tofauti vya habari na kazi zao ambazo amefanywa ziliandikwa kitaalamu kwani wengine kusubutu kutumia mikataba ya kikanda na kimataifa. Pia aliwataka waandishi hao wasifanye mahojiano marefu ili kuleta ladha zaidi katika makala zao. Alisema changamoto ambayo niliona ndani ya makala mulizofa...

JAMII YAASWA KUWEKA USIRI KWENYE MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII.

Na Nihifadhi Issa, Zanzibar. Taasisi ya Zaina Foundation imesema kuna umuhimu wa kutambua usalama wa mtandaoni ili kujilinda dhidi ya udhalilishaji au upotevu wa taarifa ambazo ni siri. Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Zaituni Njovu amesema njia moja ya usalama mitandaoni ni kuepuka kuweka wazi kila taarifa ambayo ni muhimu ikiwemo umri hali ya afya na mambo ya kifamilia. Ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari na taasisi mbalimbali namna ya kuzuia changamoto za mtandao.  “Ni vyema kutumia mitandao kwa kufuata kanuni na tahadhari ili kuwa salama na kuepukana na (cyber-crime) uhalifu wa mtandaoni” alisema Zaituni. Amesema elimu hiyo ni muhimu kwa jamii ili kuongeza ujuzi na maarifa kwa watumiai na kubaini viashiria vya uhalifu mapema. Nao washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuyafanyia kazi na kuwa mabalozi kwa wengine lengo ni kuhakikisha jamii ipo salama katika matumizi ya mitandao ambayo kutokana na dunia ilivyo hayaepukiki.

TAMWA, ZNZ yawataka wazazi kuwa Makini na watoto kipindi cha sikukuu.

C hama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kinawakumbusha wazazi na walezi kuendelea kuwalinda na kuhakikisha usalama wa watoto wao kueleekea katika sikukuu za Eid el Fitri. Ikiwa tunaingia katika kipindi cha Sikukuu, tunayo furaha kubwa kuungana na jamii katika sherehe hizi za kipekee. Lakini pamoja na furaha hii, TAMWA ZNZ tunaikumbusha jamii kutosahau majukumu yetu katika kulinda na kuhakikisha usalama wa watoto wetu. Hivi karibuni tumeendelea kushuhudia ongezeko la matukio ya udhalilishaji, kutoka matukio 1360 mwaka 2022 hadi matukio 1954 mwaka 2023, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 43.7, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Mtakwimu Mkuu ambayo pia inaonesha kuwa waathirika wengi wa matukio haya ni watoto ambapo kwa mwaka 2023 walikua ni asilimia 83.7 ya waathirika wote. Kutokana na ripoti hiyo tunasisitiza umuhimu wa kuongeza jitihada za hali na mali katika kupunguza matukio hayo kwa kuwa nao karibu na kuzifuatilia nyenendo za watoto/ vijana wao kwa ki...

AJALI YAUA WAANDISHI WA HABARI WAWILI WA MKOA WA LINDI.

WATU wawili ambao ni waandishi wa habari mkoa wa Lindi wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali . Ajali hiyo iliyohusisha gari dogo imetokea majira ya usiku wa kuamkia Leo March 26 eneo la Nyamwage mkoani mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani) Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo Alli Husein alisema Waandishi hao walikuwa wanatokea Dar es Saalam kwenye mafunzo kurejea mkoani Lindi . Waandishi waliofariki dunia ni Abdalla Nanda wa Chanel Ten mkoa wa Lindi na Josephine Kibiriti wa Sahara Media Group. M atukio Daima media kumtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani)Protasi Mutayoka amethibitisha kutokea Kwa Ajali na kuwa Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 7 usiku wa March 26 na Chanzo ni Dereva wa Centar ambae baada ya ajali alikimbia na msako wa kumtafuta unaendelea. Alisema kuwa kwenye gari ndogo ya waandishi walikuwa watu watatu na Wawili Mwanamke mmoja na mwanaume walifariki Dunia eneo la tukio na mmoja ni majeruhi amelazwa Hospitali na mguu ...