Na, Hassan Msellem, Pemba
Kijana Mbarouk Salum Mbarouk 20, Mkaazi wa Kipapo Shehia ya Chonga Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki baada ya kupata Ajali ya kugongwa na Gari akiwa anaendesha chombo Cha maringi mawili aina ya Vespa katika Eneo la Kipapo Pemba.
Tukio Hilo limetokea March 24 Majira ya saa 7 za Mchana Huko katika Eneo la Kipapo Shehia ya Chonga Mkoa wa Kusini Pemba.
Akikiri kupokea mwili wa Marehemu huyo Daktari Dhamana wa Hospital ya Chake Chake Abraham Said Msellem, amesema March 24 Majira ya saa 8:30 za Mchana amepokea Kijana anaekadiriwa kuwa na Miaka 20 ambaye alipata Ajali ya kugongwa na Gari na kuumia maeneo mbali mbali ya mwili wake ikiwemo mbele ya fuvu la kichwa mkono wa kulia.
Aidha amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alipata majeraha makubwa katika Eneo la fuvu la kichwa jambo ambalo lilisababisha kuvuja Kwa damu na kupotezea Maisha punde wakati akifanyiwa matibabu.
Ili kupata ufafanuzi juu ya ajali hiyo Mwandishi wa Habari hizi alimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba lakini jitahada za kumpata ziligonga mwamba.
Ajali za Barabarani ni Moja miongoni mwa matukio yanayotokea mara Kwa mara Visiwani Zanzibar huku Chanzo Cha Ajali hizo kikitajwa kuwa ni Mwendo Kasi, ulevi pamoja kutokuzingatia Sheria za Usalama Barabarani.
Kifo cha kijana huyo kimefikisha idadi ya watu nane kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi January 2022, katika Mkoa wa Kusini Pemba.
Habari hii niliichapisha kwenye ukurasa wangu wa Facebook March 26, 2022 kwa ushahidi wa kiungo (link) hichi kabla ya kuanzisha blog ya Pemba Post ambayo nimeichapisha habari.
Link of Facebook above👇
https://www.facebook.com/share/p/zPTMPzMppcbAfbUX/?mibextid=oFDknk
Mwisho.
Story By English.
And, Hassan Msellem, Pemba
Kijana Mbarouk Salum Mbarouk 20, Resident of Kipapo Shehia Ya Chonga District Chake Chake South Pemba Region, has died after being hit by a car while driving a Vespa in Kipapo Pemba.
The event happened on March 24 around 7 o'clock in the afternoon in the area of Kipapo Shehia of Chonga, South Pemba Region.
Acknowledging that he received the body of the deceased, Doctor Dhamana of Chake Chake Hospital, Abraham Said Msellem, said that on March 24, around 8:30 in the afternoon, he received a young man estimated to be 20 years old who had an accident when he was hit by a car and injured various parts of his body. including the front of the skull on the right hand.
In addition, he has said that the preliminary examination shows that the Deceased suffered serious injuries in the area of the skull which caused bleeding and lost his life soon while undergoing treatment.
In order to get an explanation about the accident, the reporter of this news looked for the South Pemba Regional Police Commander, but efforts to find him were unsuccessful.
Road accidents are one of the events that occur regularly in the Zanzibar islands, with the cause of these accidents being speeding, drunkenness, and disregarding Road Safety Laws.
The death of the young man has reached eight people in a period of three months from January 2022, in the South Pemba Region.
The End.

Comments
Post a Comment