Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MSIBA

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

MWANAHABARI TEMMY MAHONDO AFARIKI DUNIA.

Mwanahabari Temigunga Mahondo amefariki Dunia Hospital ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. Mahondo alikuwa mwandishi wa habari na meneja wa kituo kikongwe cha Radio cha Country Fm cha mkoani Iringa na baada ya hapo alifanya kazi na taasisi za kimataifa za kihabari kama mkufunzi kwa wabahabari. Mahondo pia amekuwa msaada mkubwa kwa chombo cha Matukio Daima Media kwani hadi mauti yanamkuta ndie alikuwa mkuu wa kitendo cha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi katika Matukio Daima Media . Mahondo pindi alipolazwa Hospitali ya Mlonganzila wanakundi wa Iringa Daima ambako alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo ambalo Admin wake mkuu ni mkurugenzi wa Matukio Daima Media Francis Godwin walimchangia zaidi ya Tsh milioni 3 na yeye alitoa sehemu ya pesa hiyo kuchangia ujenzi wa ICU Hospital ya Rufaa ngazi ya mkoa ya Tosamaganga pesa alizokwenda kukabidhi mwenyewe na baadhi ya wanakundi huku akihamasisha jamii kuchangia zaidi. Siku nne kabla ya kifo chake uongozi wa Iringa Daima ulikwenda kum...