Kukosekana Udhamin ligi za wanawake wadumaza maendeleo ya michezo.

Na, Amina Mchezo.



Udhamini ni chachu ya kulifanya jambo au shughuli Kwa urahisi na Kwa uhakika wa hali ya juu.


Udhamini inategemea na namna ya makubaliano yenu haijalishi iwe fedha, ama bidhaaa au vifaa ilimradi unahakikisha unafanya jambo lako likiwa na usimamizi kamili.


Udhamini katika michezo unatoa fursa na hamasa ya wachezaji kuona Wanapata heshima na kuwekewa sawa maslahi yao pamoja na clabu yao.


Wadau mbalimbali wa michezo wamesema timu za wanawake hazina udhamini kutokana na kukosa mvuto  kutokana na wanawake wengi Kwa Zanzibar hawana mwamko wa kimichezo.


Wameendelea kusema kuwa Kwa Zanzibar wanawake kucheza mpira imekuwa na mitazamo tofauti na ndio maana wadau wengi wanashindwa kuwekeza fedha zao katika timu au ligi za wanawake.


Wakizungumza na mwandishi wa makala hii wadau hao wamesema udhamini wowote unatakiwa uwe na faida pia Kwa pande Zote huku mdhamini akitumainia kutangaza biashara, taasisi au kampuni yake.


"Unajua Kila kitu ni mwamko wa watu uwanjani na ndio unaosababisha wadau waweze kudhamini michezo ila Kwa wanawake ni tofauti" Wamesema wadau.


Wachezaji wa Timu za wanawake wamelalamikia vikali hali ya kukosa udhamini Kwa timu zao wakidai kuwa bado viongozi wa juu hawajawa tayari kuzipa nguvu ligi za wanawake Kwa kukosa kuwapa ushirikiano kama ligi za wanaume.


Wamesema wanachohitaji ni kipaumbele ambacho kitawasaidia hata wao kuuzika Kwa timu za nje.


Wachezaji wa timu ya Warriors na timu ya woman Fighter ya wanawake wamesema mpira ni ajira kama ajira nyengine hivyo wanaamini na wao wanawake wanaweza kuwa miongoni mwa wenye kupata ajira kupitia michezo.


"Timu zetu udhamini mdogo au haupo kabisa na ndio maana tunashindwa kujiendesha na kuzalisha timu nyengine mitaani hali inayotutia unyonge kimichezo" Wamesema.


Ali Hamadi ni miongoni mwa makocha wa timu za wanawake amesema timu zinakosa wadhamini Kwa sababu kwanza walimu wenyewe hawajawapa kipaumbele.


Amefahamisha kuwa timu za wanawake wakati wa mashindano wanashindwa kuandaliwa mapema ili kuh⁶pambana kiushindi katika mashindano hayo.


Hamad amebainisha kuwa hata wanajamii bado hawajawa tayari kumkuza mtoto wa kike kimichezo kutokana na kumuona kuwa sio mahala pake huku wakitoa fursa zaidi Kwa watoto wa kiume.  


Amesema Kwa Sasa wamekuwa wakitafuta wadau mbalimbali kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za wanawake katika michezo Kwa maendeleo huku wakitoa elimu Kwa wanajamii.


" Naishauri serikali wazidi kushajihisha clabu za wanawake kushiriki katika mashindano mablimbalinana hata ligi za shule pia washirikishwe"  Ameongeza.


Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar ZFF Hussein Ahmad Vuai amesema wamekuwa wakifanya Kila hali ili timu au ligi za wanawake zipate udhamini ila bado wadhamini wamekuwa wagumu kuwekeza kwao.


"Inawezekana ikawa Kuna sababu labda ya mwamko mdogo wa ushiriki Kwa wanawake katika michezo na ndio maana wadhamini hawako tayari kutoa ushirikiano "Amesema katibu.


Amesema hali hiyo si Kwa wao tumu kama timu Bali hata shirikisho limekuwa likipata wakati mgumu katika kuendesha ligi za wanawake. 


Katika kuona soka la wanawake nalo linapata udhamini wa Uhakika chama Cha waandishi wa habari wanawake Tamwa Zanzibar wamekuwa na utaratibu wa kuandaa mafunzo Kwa waandishi wa habari ili kupaza sauti zao kwenye vyombo vya habari katika kuvutia wawekezaji kwenye michezo.


Khairat Ali ni afisa miradi kutoka Tamwa Zanzibar amesema Kwa Sasa wanatekeleza program za Michezo Kwa maendeleo Kwa waandishi wa hanari lengo likiwa ni kuandika habari Kwa wingi za Michezo Kwa wanawake.


Amesema Kila zinapotolewa taarifa nyingi za wanawake ndio wadau na wadhamani watajua kazi na kile kinachofanywa nawanamichezo wanawake. 


"Tunajua kwamba Kila kitu kikiwa na hadhira kubwa ndio wafanyabiashara ama wafadhili Wanapata moyo wa kwenda kufanya udhamini kwenye masuala ya michezo. " Amesema Afsa Khairat.


Khairat ameongeza kuwa inaonekana bado Kwa waandishi wa habari hawajatimiza wajibu wao Kwa kusaidia michezo Kwa wanawake Zanzibar.


"Juzi tulikuwa na kongamanono la kimataifa la


Comments

Popular posts from this blog

MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba

Mtangazaji wa Wasafi Media, Dida Afariki Dunia