Skip to main content

WASEMAJI WANAWAKE KWENYE TIMU WAONGEZA HAMASA MICHEZONI.

Na Amina Mchezo 

Uhamasishaji michezoni unatokana na uwepo  wa watu maalum ambao hutumia muda wao mwingi kutafakari namna gani ya kuwaleta watu karibu na Kwa mbinu gani.

Michezo kikawaida huhitaji mvuto mkubwa Kwa jamii kwani uwepo wake huleta furaha na kujuana na watu mbalimbali.

Maafisa habari kwenye michezo wananafasi kubwa ya kutoa taarifa zinazohusu vilabu na wanachama wengine.

Inaelezwa kuwa ili upatiwa leseni ya timu yako na shirikisho la mpira wa miguu ni lazima uwe umetimiza vgezo ikiwemo kipengele Cha kuwa na afisa habari wa timu.

Huku cha kusikitisha zaidi ni Kuona timu ambazo zinategemewa kibeba Zanzibar hata hawaoni umuhimu. kuwa na afisa habari.

Hadi Sasa maafisa wa habari wanawake katika michezo ni wawili tu Kwa Zanzibar huku Timu Zote 16 znazoshiriki ligi kuu Zanzibar hakuna timu yenye msemaji mwanamke, wakati ligi daraja la kwanza Kanda ya unguja timu Moja tu kati ya timu 18 ndio yenye msemaji mwanamke na timu Moja tu ilio mkoa ndio yenye msemaji mwanamke. 

Hali hii si Kwa wanawake wenyewe Bali hata wadau mbalimbali wa michezo wanaona ni khatari katika kuupoteza ushiriki wa wanawake michezoni.

Nd. Ali Khamis na nd. Mtumwa Mzee ni wadau wa michezo Zanzibar wamekuwa wakifuatilia Kwa karibu sana maafisa wa habari wanawake walio nje ya Zanzibar na kufanya vizuri kwenye vilabu vyao katika kuleta hamasa za michezo.

"Dunia Kwa Sasa inamuhitaji mwanamke katika Kila nyanja hivyo wanawake kwenye michezo wanaongeza mvuto Kwa wanawake wengine lakini pia ni fursa kwao katika mapambano" Wamesema.

Wameendelea kusema kwamba Kwa upande wa Zanzibar wanawake wengi wamekuwa na hofu ya kuchukua jukumu la kuisemea timu hasa za wanaume ingawa wakipewa nafasi wanafanya vizur.

Zainab Haroub Mohd ni afisa habari wa kwanza mwanamke katika michezo alikuwa aliisemea timu ya Kilimani city ilikuwa daraja la kwanza Kanda amesema uwamuzi wake uliibua hisia kubwa na kuwafanya wanawake wengine kutamani kuwa katika nafasi hiyo.

Zainab amesema uwepo wake kwenye timu ulileta tija kubwa kutokana na utofauti wa kiongozi huku mashabiki na wadau wakivutiwa nae.

Amebainisha kwamba mwanamke kuwa afisa habari wa timu za mpira wa miguu hasa za wanaume sio sababu ya kujivunjia heshima huku akisifu ushirikiano anaopatiwa kutoka Katika uongozi wa timu yake.

"Najivunia Sana kujitoa kwangu kuwa msemaji wa timu za michezo Zanzibar kumevutia wanawake wengi kuwa wanamichezo na kuona kumbe nao ni sehemu ya ushiriki wao" amesema Zainab 

Kazija Thabit Vuai msemaji wa timu ya Ras Kazoni ya wanaume ilio daraja la kwanza Kanda ya unguja nae amebaisnisha fursa wanazozipata hasa za uvutiaji wa mashabiki katika timu.

Amesema ingawa timu hiyo Haina mashabiki wengi lakini uwepo wake ulionesha hamasa Kwa wachezaji wakiamini mwanamke ana ushawishi mkubwa wakati akitoa taarifa za timu husika.

"Yaani nikipata changamoto ya kutokuwepo kwangu uwanjani wachezaji wengi na viongozi wa timu hunipigia kunieleza bila uwepo wangu hakuna hamasa ya kutosha" amesema Kazija.

Kazija amebainisha kwamba ushiriki wa mwanamke katika michezo hakumpelekea mwanamke huyo kuvunjiwa heshima endapo atajiheshimu. 

Kepteni wa timu ya Raskazoni Ramadhani Yussuf Issa maaruf OK amesema timu yao kuwa na msemaji mwanamke wanajivumia Sana huku wakisema wanatamani afisa wao huyo aendelee zaidi na zaidi

Ramadhani amesema wanamuangalia kazija kama mwanamke mwenye thamani kubwa kubwa Sana kwani amekuwa akifanya kazi Kwa kujitoa na kuhakikisha timu yake inakuwa Bora katika ligi.

"Afisa wetu Kwa kweli tinajitajidi kwenda nae vizuri na timu nyengine nazo pia hutuonea choyo kutokana na kumuona ana tumia nafasi yake vizur ya kuisemea timu yetu na imekuwa Kila mara ikisikika kupitia vyombo vya habari.

Mbali ya maafisa hao wa habari ama wasemaji wa timu za michezo wanawake kufurahia kazi wanayoifanya huku wakiona Ina tija Kwa namna Moja au nyengine lakini zipo timu ambazo zilikuwa na maafisa wanawake na baadae kuachia ngazi.

Kujiuzulu Kwa baadhi ya maafisa wa habari wanawake nao Kuna sababu kadhaa kama alivyoelezea bi Mwajuma Juma akise

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...