Skip to main content

Elimu na miundombinu rafiki inahitajika katika kukuza ushiriki wa jinsia zote katika michezo- Tumbatu

 SHEHA wa Tumbatu Uvivini ndugu Ngwali Sheha Haji, amesema miongoni mwa changamoto zinazopelekea kutokuwepo ushiriki sawa wa kijinsia katika michezo ni pamoja na kukosekana kwa miundo mbinu rafiki na skuli kutokua na muda maalum wa michezo kwa wanafunzi.


Sheha Ngwali amesisitiza kuwa mila na desturi sio kikwazo kwani historia inaonesha kuwa kuna wanawake mbalimbali kutoka kisiwani hapo ambao wamewahi kushiriki michezo na kuwa vinara katika kisiwa hicho.



“Hapo zamani miaka ya 1973 wakati mimi ni mwanafunzi kulikuwepo wanawake wanaoshiriki michezo na kuchukua medali nyingi lakini ushiriki umepungua kutokana na changamoto za ukosefu wa mazingira rafiki ya kushiriki michezo kwa watoto wa kike”, alisema Sheha Ngwali.



Nae Mwalimu mkuu msaidizi skuli ya Tumbatu Msingi “A” ameeleza kuwa skuli hiyo ina mikakati ya kuwahamasisha watoto wa kike kushiriki michezo hususan baada ya kukamilika viwanja rafiki vya michezo kupitia mradi wa michezo kwa maendeleo



Kwa upande wa wanafunzi wa kike wanaoshiriki michezo hasa mpira wa mikono (netball) katika skuli hiyo wamesema kushiriki kwao katika michezo kumewasaidia kuimarisha afya zao, kutembea sehemu mbalimbali pamoja na kupata zawadi.



Pia wameiomba serikali na wadau mbali mbali kuwaunga mkono kwa kuwasaidia vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jezi na vyenginevyo ili iwe rahisi kwa wao kushiriki katika michezo.



Katika muendelezo wa utekelezaji wa mradi wa michezo kwa maendeleo, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ) kimefanya ziara maalum pamoja na waandishi wa habari kutembelea kisiwa cha Tumbatu kuangalia hali ya michezo katika kisiwa hicho.



Akizungumza katika ziara hiyo mkuu wa kitengo cha mawasiliano TAMWA ZNZ Sophia Ngalapi amesema kazi kubwa ya TAMWA ZNZ ni kutetea haki za wanawake na watoto pamoja na kukuza usawa wa kijinsia katika kila sekta ndani ya jamii.



Ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuangalia hali ya kimichezo ndani ya kisiwa cha Tumbatu ikiwemo ushirikishwaji wa jinsia zote katika michezo, miundo mbinu pamoja na kupata maoni kutoka kwa wakaazi wa kisiwa hicho juu ya ushiriki wa watotot wa kike katika michezo bila kuharibu mila, desturi na silka za wazanzibari.



Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...