Skip to main content

"Hata Dini zetu zimehimiza kushiriki michezo Ili kuwa na afya imara" Othman Massoud Othman

Na, Hassan Msellem, Pemba



MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, amevishauri vilabu ya mazoezi nchini, kujitengenezea kanuni, zitakazowavutia watu wingi zaidi kujiunga kwenye mazoezi, ili kuondoa dhama potofu ya mazoezi ni uhuni.


Alisema, kama kundi kubwa la watu wanadhana kuwa mazoezi ni uhuni na kuvunja maadili, ni wakati sasa kwa vilabu vya mazoezi na michezo, kuwa na kanuni zitakazofuta dhana hiyo.


Makamu huyo wa Kwanza, aliyasema hayo leo Julai 28, 2024 uwanja wa michezo Gombani Chake chake, kwenye bonanza la miaka 10, tokea kuanzishwa kwa ‘Gombani Fitness Club’ lilioandaliwa kwa pamoja na TAMWA-Zanzibar na Shirika la Bima.


Alieleza kuwa, kwa vile mozoezi ni jambo muhimu kwa kila mmoja, ni vyema kuwepo na kanuni ndogo ndogo, ambazo zitawavutia wengine, kushiriki katika kupata kinga ya miili yao.


Alifahamisha kuwa, ni kweli kama kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili, inaweza kuwa sababu kwa baadhi ya watu, kuona sio sehemu salama, ingawa zikiwepo kanuni zitawavutia wengi.


‘’Kama mlivyosema kuwa, moja ya changamoto zenu ni kuwepo kwa dhana potofu, kuwa mwanamke anapofanya mazoezi au kushiriki michezo ni uhuni, sasa ili kuliondoa hili andaeni kanuni zenu,’’alishauri.


Katika eneo jingine, Makamu huyo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, aliitaka jamii kurudi kwenye vyakula vya asili, ili kujipunguzia magonjwa.


Alieleza kuwa, kwa mfumo wa maisha ulivyo sasa, na aina ya vyakula vilivyopo, ni lazima sasa jamii irudi kwenye vyakula vya asili, ili kupunguza ukali wa magonjwa.


‘’Wengi wetu tunavyovitambi sugu, mazoezi hatutaki, basi japo kurudi kwenye vyakula vya asili, ambavyo kwa kiasi kikubwa, havisababisha magonjwa ya moja kwa moja,’’alishauri.


Akizungumzia faida za mazoezi, alisema ni kupunguza magonjwa ambayo pamoja na matumizi ya dawa, lakini yanapungua nguvu, kwa kufanya mazoezi.


‘’Faida nyingine ya mazoezi ni kujenga umoja, mshikamano wa kweli, baina ya mtu na mtu na hata klabu moja na nyingine,’’alifafanua.


Kuhusu miaka 10 ya ‘Gombani Fitness Club’ Makamu huyo wa Kwanza, aliupongeza uongozi, kwa kuendelea kuwalea wanachama na kufikia malengo yao.


‘’Hili mlilolianzisha ni jambo muhimu mno, na mimi nitakuwa balozi nzuri kwa wenzangu, kuwaelekeza namna ya kuwa na vilabu vingi zaidi, vyema wanachama wengi,’’alifafanua.


Mwenyekiti wa Gombani Fitness Club Hamad Ali Malengo, alimshukuru Makamu huyo wa Kwanza, kwa kukubali kushirikiana nao, katika sherehe hizo za miaka 10 ya taasisi yao.


Aidha, alisema wamekuwa wakishirikishwa na kushirikiana kwa karibu na serikali za mkoa wa wilaya, katika shughuli kadhaa za kitaifa.


Akisoma risala ya kwa niaba ya Shirika la Bima Zanzibar Afisa Program wa mradi wa michezo kwa maendeleo kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar Hairat Haji, alisema wamekuwa wakiihamasisha jamii, kuwa michezo ni kwa wote.


Alisema, mradi huo kwa sasa unatekelezwa na Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ‘ZAFELA’ Kituo cha mijadiliano kwa vijana ‘CYD’ pamoja na TAMWA-Zanzibar kwa ufadhili Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani ‘GIZ’


Alifafanua kuwa lengo kubwa, ni kuongeza ushiriki wa wanawake na watoto wa kike, katika mazoezi na michezo, kwani kila mtu, anayo haki sawa, hasa katika eneo hilo.


‘’Katika kufanikisha mradi huu, sisi TAMWA jukumu letu ni kuwawezesha waandishi wa habari kimafunzo, na kisha wawe weledi wa kukuza usawa wa kijinsia na ujumuishi katika michezo, kupitia kazi zao,’’alieleza.


Aidha alisema, tayari waandishi wa habari 30 wa Zanzibar, wameshawezeshwa namna bora ya kuandika habari na kutengeneza vipindi, vinavyoelezea fursa sawa ya michezo na eneo la ujumuishi.


Kuhusu changamoto, alisema zilizoibuliwa ni kuinasibisha michezo na mazoezi kwa mtoto wa kike na wanawake, ni uhuni, jambo ambalo sio sahihi.


‘’Jingine lililoibuliwa na waandishi wa habari, ni ukosefu wa miundombinu rafiki, ughali wa vifaa vya michezo pamoja na dhana ya utamaduni,’’alieleza.


Mapema Mwenyekiti wa Umoja wa vilabu vya mazoezi Zanzibar ‘ZABESA’ Said Suleiman Said, alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa, moja wapo ikiwemo ukosefu wa eneo mahasusi la kufanyia mazoezi.


Awali Mkuu wa wilaya ya Chake chake Abdalla Rashid Ali, alisema Gombani Fitness Club, imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali.


Awali Makamu huyo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, aliungana na vilabu zaidi ya vitano vya mazoezi kutoka Unguja, Tanga na wenyeji Pemba, katika matembezi ya kilomita tatu, yalioanzia mjini Chake chake hadi uwanja Gombani.


‘’Inapotokezea shughuli za kitaifa, hushiriki kwenye usafi, uchangiaji damu, jambo ambalo linatupa moyo kuona wanajali serikali yao bila ya ubaguzi,’’alisema.




Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...