"Tuhamasishe watoto wa kike kushiriki michezo kuleta usawa wa Kijinsia katika sekta zote" Afisa Programu Tamwa, ZNZ
Na, Thuwaiba Habibu, Unguja
Katika kuazimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike duniani, wadau wa michezo kwa maendeleo Zanzibar ambao ni Jumuiya ya wanasheria wanawake, Zanzibar (ZAFELA) kituo cha mijadala kwa vijana (CYD)na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,ZNZ) kwa kushirikiana na shirika la Ujerumani (GIZ) imeandaa shughuli mbali mbali za michezo kwa maendeleo ili kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike na ustawi wa kijinsia katika michezo.
Akitoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari Afisa Program wa michezo kwa maendeleo kutoka Tamwa Zanzibar, Khairat Haji amesema maadhimisho hayo yatawashirikisha wanafunzi kutoka skuli mbali mbali za msingi za mkoa wa kaskazini 'A', Mjini ,na Magharibi 'A', na yataanza kwa michezo ya mpira wa pete (Netball) za kirafiki zitakazo husisha timu za watoto wa kike kutoka tumbatu, jongwe,mkokotoni,mto wa pwani, kianga,mtoni , kiembe samaki B' na uroa.
Alisema kuwa shughuli nyengine zitakazo fanyika ni ziara kwenye skuli mbali mbali ili kuendeleza michezo kwa maendeleo (S4 D) ambayo itawafundisha wanafunzi namna ya kujikinga dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na kuelimisha kuhusu masuala ya wanawake na uongozi.
Amesema kuwa,Wanafunzi pia watashiriki kwenye uchoraji wa picha ambazo zitaakisi maudhui ya S4D ambayo itawapa fursa ya kuelezea mawazo yao, kuhusiana na michezo na usawa wa kijinsia.
Aidha Afisa huyo, amesema kuwa,kilele cha maadhimisho hayo, kitafanyika siku ya jumamosi oktoba 12 mwaka huu,ambapo zitachezwa mechi za fainali ya mpira wa pete,na pia picha zilizochorwa na wanafunzi hao, zitagaiwa kama zawadi.na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto, mheshimiwa Anna Athanas Paul ambae ataongoza shughuli ya kugawa zawadi kwa washiriki wote.
Aidha amesema kuwa, maadhimisho hayo yanalenga kuinua ari ya watoto wa kike kushiriki michezo, kupinga ukatili wa kijinsia na kuboresha usawa wa kijinsia visiwani Zanzibar.
"Tunaamini maadhimisho hayo ni sehemu ya mikakati ya wadau wa SFD Zanzibar,wa kuendeleza uawa wa kijinsia na haki za mtoto wa kike kupitia michezo"" alisema.
Nao, waandishi walioshiriki katika kikao hicho, waliuliza kuwa wamezingatia vigezo gani katika kuzipata hizo shule zitakazo shiriki katika madhimisho hayo.
Akijibu suala hilo, Afisa kutoka CYD Rahma Juma amesema, kuwa katika programu hiyo wanashirikiana na Serikali hivyo, uteuzi wa shule hizo umefanya na Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar.
Comments
Post a Comment