Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2026

JELA JELA MIAKA 60 KWAJELA MIAKA 60 KWA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 16.

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Mahakama ya Kupambana na Makosa ya Udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake, Jana April 14 imemuhukumu kutumikia Chuo cha Mafunzo Ismail Ussi Makame miaka 19, mkaazi wa Mikarafuuni kwa makosa mawili ya Ubakaji. Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Taki Abdalla Habib, imeelezwa na mwendesha Mashtaka Asia Ibrahim Mohamed, kuwa tarehe 19.12.2025 saa  7:00 za usiku huko Kinyasini Mkoani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, mshtakiwa alimbaka msichana wa miaka 16 baada ya kumtorosha msichana huyo kutoka nyumbani kwao na kwenda nae sehemu anayolala, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 108(1)(2) na 109(1) Shehia ya adhabu Sheria Nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar likiwa ni kosa la kwanza. Katika kosa la pili, tarehe 20.12.2025 saa 7:30 za usiku mshtakiwa alimbaka tena msichana huyo. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mahakamani hapo  06.01.2026 na idadi ya mashahidi 6 walitoa ushahidi ambao haukuacha chembe ya shaka, hivyo Mahakama...