Skip to main content

GHARAMA ZA VIFAA VYA MICHEZO, KIKWAZA KWA WANAWAKE KUSHIRIKI MICHEZO.

 NA, SALIM HAMAD, PEMBA

Gharama za Vifaa vya Michezo ni miongoni mwa kikwazo kinachowafanya wanawake kushiriki michezo mbali mbali Kisiwani Pemba.

WAKATI Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi mbali mbali za kiraia nchini ikiwemo Chama Cha Waandishi wa Habar wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA) zikielekeza nguvu zake katika kuhamasisha wanawake kushiriki michezo, ingawa bado kumekuwa na kikwazo katika upatikanaji wa vifaa vya michezo.

Michezo ni jambo zuri ambalo limekuwa na umuhimu wa kipekee katika kuimarisha afya za wananchi.

Pia michezo ni suala ambalo serikali na wadau wengine wamekua wakielekeza nguvu zao na kuekeza katika sekta hiyo, hivyo imekua ni kichocheo kikubwa cha kupata fursa ambazo zinaweza kuinua uchumi wa wanamichezo.

Kutokana na umuhimu wa michezo hata jukwaa la Beijing kupitia mkutano ulioandaliwa na shirika la UN Women likishirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, wakati wa vikao vya 59 vilitambua pia umuhimu wa michezo na elimu ya mazoezi ya mwili katika kuweka bayana nyota ya wanawake na wasichana.

Jukwaa hilo la Beijing lilitambua pia umuhimu wa michezo na elimu ya mazoezi ya mwili katika kuweka bayana nyota ya wanawake na wasichana.

Pamoja na juhudi hizo zinazochukuliwa katika kuhamasisha wanawake kushiriki michezo, bado wanamichezo wanawake walia juu ya ghara kubwa za vifaa vya michezo kama vile Viatu, na mavazi kwa ajili ya kuchezea.

WANAMICHEZO WENYEWE

Kulthum Ali Khamis mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Timu ya Wete star (WOMEN CLUB) mkaazi wa Mgogoni Wilaya ya Wete Pemba anasema vifaa vya michezo bei zake ni kubwa, kwani kiatu hasa cha mazoezo kinachokubalika ni shilingi Elfu 60,000/= au 40,000/= hivyo bei hiyo ni kikwazo kwao.

‘’Kwakweli gharama za vifaa vya michezo nikikwazo kwetu, kwani tunatakiwa kuwa na viatu Jezi na mipira, lakini vinashindwa kununua, bei ni kubwa,’’anaeleza.

Alisema ni vyema wadau wa michezo kuziangalia timu za michezo za wanawake kwa kuwapatia vifaa, ili waweze kuendeleza vipaji vilivyomo katika timu zao.

Alisema kuna haja kwa Serikali kuangalia kwa pande zote katika uwezeshaji wa Vifaa kwani jambo hilo litawafanya wanawake kuhamasika kuingia kwenye michezo.

‘’Sisi tunashindwa kuingia katika michezo mana bei za vifaa ni gaharama mana bado hapa hapajawekwa mazingira wezeshi ya utolewaji wa vifaa hususani kwa akinamama tunaomba Serikali na wadau wengine hili waliangalie kwa karibu’’alisema.

Fatma Mkubwa Mohamed mchezaji wa mpira wa mikono kutoka timu ya wanawake wenyeulemavu Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba anasema gharama za michezo ni moja ya kikwazo kinachokwamisha timu zao kushindwa kuendelea.

 Anasema kutokana na Maisha walionayo kwa sasa katika timu zao wanashindwa kumudu kununua gharama za vifaa kama vile viatu, mipira.

‘’Tunapokuwepo uwanjani tunatakiwa kila mchezaji awe na mpira wake kwa ajili ya kufanyia mazoezi, lakini inaua ni ngumu hatuwezi kunua gharama ni kubwa alieleza,’’

 ni vigumu kwa mtu kupambana hata atakapoipata helo kama elfu thelathini au arobaini ni vigumu kuitoa kutokana na hali za Maisha.

Tamasha Ali Khamis Kocha wa timu ya mpira wa miguu ya wanawake kutoka Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba (Women Club) anasema suala la michezo ni gharama hasa kwa mchezaji ambaye hajafika mbali mara nyingi imekuwa anajitegemea.

Alifafanua kuwa Pamoja na kuwa baadhi ya wanawake wanamuamko katika kushiri michezo, bado kumekuwepo na ghara za vifaa ikiwa ni moja ya sababu inayorejesha nyuma ndoto zao kwenye harakati za michezo.

Hata hivyo aliomba wadau kuangalia kwa karibu vifaa vya michezo hususani kama hile ya bask ball na ahata Volbol ambayo mara nyingi wanawake wamekuwa wakijikita kwenye michezo hiyo.

 ‘’Wapo baadhi ya wanawake wamekua na mwamko wa kupenda michezo lakini bado hakuna mazingira mazuri ya kuwezeshwa masuala ya vifaa vya michezo,’’anaeleza.

Hamida Juma Amani mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Mkoani anasema licha ya kikwazo hicho cha gharama za michezo, ataendelea kushiriki michezo kwani ni suala ambalo limo ndani ya damu yake.

“mimi nikiwa ni kijana wakike nitaendelea kwenye michezo kwani ndio kipaji change na napenda sana kwenye hii tasnia ya Michezo’’amesema.

Ali Miraji ni Muuzaji wa Vifaa vya Michezo katika Mji wa Chake Chake amesema ni kweli Vifaa vya michezo bei zake zipo juu na kwamtu wa kawaida anaweza kushindwa kumudu gharama za ununizi.

Ameeliza Vifaa kama mpira unauzwa kwa shiling elfu 40000 huku Viatu Vikiuzwa elfu 60000 gadi zinauzwa kwa shilinfgi 3500.

Hivyo kutokana na hali hiyo inaweza kuwa kikwazo kwa wanawake kushiriki michezo kwani hawana njia ya kujipatia kipato ya kuweza kumudu gharama hizo.

Ofisa Mdhamini Wizara ya Habari Pemba amesema Wizara italiangalia kwa karibu suala la vifaa katika kusaidia wanamichezo ingawa kwa sasa Wizara inatengeneza mazingira Rafiki ya Viwanja.

Amesema Wizara inajenga Viwanja Vya Michezo kwa Kila Wilaya vikijumuisha na Michezo ya wanawake ili kuona na wao wanapata fursa ya kujikita kwenye michezo 

 ‘’Ni kweli kuna changamoto ya Vifaa vya Michezo hususani kwa wanawake lakini wizara inaendelea kuweka mazingira Rafiki ya kuona kila mmoja kwa jinsia yake anapata kushiriki michezo’’alisema Mfamau.

SHIRIKISHO LA SOKA ZANZIBAR (ZFF)

Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar Ofisi ya Pemba (ZFF) Khamis Hamad Juma amesema katika Ofisi yao wamekua wakisaidia vifaa kwa upande wa timu za wanaume.

Amesema kwa sasa shirikisho hilo litahakikisha wanawasaidia timu za michezo ya wanawake , ikiwemo gharama za vifaa vya michezo ili kuona wanaondokana na changamoto hiyo na waweze kukuza timu zao.

‘’Tutahakikisha tunaziwezesha timu za michezo za wanawake, ili kuona na wao wanajipatia fursa mbalimbali zitokanazo na michezo,’’alieleza.


 MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...