Skip to main content

"TUNAOMBA USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI, WANAWAKE WAGOMBEA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI" ZAMECO

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA

KAMATI ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) imeiomba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhakikisha usalama wa Waandishi wa Habari, Wanawake wagombea, na Wasimamizi wa Uchaguzi (Mawakala) katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar ambao utafanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Kamati hiyo imesema inatambua kuwa mazingira salama kwenye masuala muhimu yenye maslahi mapana na mustakabali wa nchi hususan suala la uchaguzi, ni sharti la msingi ili kuhakikisha kila mdau anatekeleza majukumu yake kwa uhuru na bila ya hofu kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 15(1) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984:

"(Kila mtu anastahiki kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na ya nyumbani kwake, na pia heshima, na hifadhi ya maskani yake na mmawasiliano yake)."

Aidha Kamati imesisitiza kuzingatiwa hatua mahsusi kwa mujibu wa sheria na kanuni za kulinda haki na usalama wa makundi haya wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi huku ikisisitiza kuwa  waandishi na jamii kwa ujumla, wanahaki ya kupewa  fursa ya kupata taarifa bila ya kuingiliwa kwani kila mmoja ana haki hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Zanzibar 1984 sambamba na ibara ya 19 ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binaadamu (UDHR-1948) inayoeleza “Kila mtu ana haki ya kuwa na maoni na mawazo yake bila ya kuingiliwa.

Aidha ZAMECO,  imesisitiza umuhimu wa Waandishi wa Habari kupewa nafasi sawa zisizo na ubaguzi katika kupata taarifa sahihi zinazohusu uchaguzi pamoja na kupatiwa vitambulisho maalum vinavyotolewa na Tume ya Uchaguzi na kuepuka kutoa fursa zaidi kwa vyombo vya Serikali na kuvikwepa vyombo visivyokuwa vya Serikali hali itakayopelekea kufuatilia na kuripoti matukio ya uchaguzi kwa weledi usawa  bila ya kuathiriwa na vikwazo visivyo vya lazima.

 Hata hivyo,  kamati imetoa mapendekezo kwa  Tume ya Uchaguzi kutoa mafunzo maalum kwa waandishi wa wabari kuhusu uandishi wa taarifa za uchaguzi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia weledi na maadili ya taaluma kwani mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha uelewa wa waandishi katika kuripoti kwa kuzingatia wagombea wa  jinsia zote.

Katika hatua nyengine, ZAMECO inapongeza ahadi iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ya kutoa na kuchapisha takwimu za jinsia za washiriki wa uchaguzi, iikiwemo idadi ya wanawake na wanaume watakaogombea nafasi mbalimbali ikiwemo Irais, Uwakilishi na udiwani pamoja na wapigakura na washiriki wa mchakato mzima wa uchaguzi ambapo takwimu hizi zitakuwa nyenzo muhimu katika kufuatilia uwiano wa kijinsia na kkusaidia kufikia lengo la usawa wa asilimia 50/50 nchini.

ZAMECO inahitimisha  kuwa, uchaguzi huru  wa haki na jumuishi unahitaji mazingira salama taarifa sahihi, na upatikanaji sawa wa fursa kwa wanawake na wanaume ili  kuimarisha  demokrasia na mshikamano nchini.


 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...