NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA
Afisa programu ya mapitio ya Sheria za Habari na Uhuru wa Habari na kujieleza kutoka Tamwa, Zanzibar Zaina Abdalla Mzee, amesema licha ya Wanaharakati, wadau na waandishi wa Habari Visiwani Zanzibar kupaza sauti juu ya kufanyiwa marekebisho Sheria za Habari suala ambalo bado halijafanyiwa kazi ipaswavyo ingawa Baraza la Wawakilishi limeahidi kulifanyia kazi suala hilo katika msimu ujao wa vikao vya Baraza hilo.
Akiwasilisha
ripoti kwa Waandishi wa Habari katika Ofisi za Tamwa Mkanjuni Pemba jana Tarehe 24\07\2025, ripoti yenye lengo la kuonesha hali halisi iliyofikiwa kwa kipindi cha miaka
miwili ya utekelezaji wa mradi wa miaka miwili unaofadhiliwa na Shirika la #CommonWealth, ripoti iliyoonesha kuwepo kwa Sheria kandamizi kwa vyombo vya Habari,
wanahabari na uhuru wa kujieleza kwa wananchi Visiwani Zanzibar.
"Miongoni mwa matokeo (Outcomes) ya mradi huu ni pamoja na kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuzitambua Sheria za Habari kuona mapungufu yaliyomo katika Sheria hizo, kutoa mapendekezo ili ziweze kufanyiwa marekebisho" alisema
"Kwa upande wa shughuli ambazo tumezifanya ni pamoja na kuandaa mikutano na wadau mbali mbali wa Habari kama vile watendaji wa Serikali na viongozi wa kisiasa hasa wale ambao tunawaona mara kwa mara wanazungumzia suala Uhuru wa Habari wakiwa katika vikao vya Baraza na mpaka Baraza la Wawakilishi linamaliza muda wake kuna ahadi kuwa katika vikao vijavyo vya Baraza hilo Sheria mpya ya Habari litajadiliwa ipaswavyo" alinena
Nae, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tamwa, Zanzibar Mohammed Khatib Mohammed, amesema kuimarika kwa Uhuru wa Habari hutegemea na Sheria za Habari zilizo rafiki kwa Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha amesema katika utekelezaji wa mradi huo wamegundua kuwa upatikanaji wa Sheria mpya za Habari sio jambo rahisi kutokana na Serikali kuchelea kufanyia kazi malalamiko ya wadau wa Habari na Waandishi wa Habari kuomba kufanyiwa marekebisho Sheria za Habari zinazowanyima Waandishi fursa ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi sambamba na Wananchi kupata fursa ya kutoa maoni.
"Kuimarika kwa Uhuru wa Habari inategemea na Sheria za habari iliyopo, kama Sheria ya Habari ni mzuri basi Uhuru wa Habari utakuwepo na kama ni mbaya Uhuru wa Habari hautokuwepo" aliongoza
Nao Waandishi walioshiriki katika mkutano huo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa mradi, wamesema licha ya kuandika habari, makala na Vipindi mbali mbali vinavyohusu kupiga chapuo uhuru wa Habari, bado wanakumbana na changamoto ikiwemo vitosho, dharau pamoja na kukosa mashirikiano kwa baadhi ya watendaji wa Serikali wakati wanapohitaji taarifa katika Habari mbali mbali zenye kuleta maslahi kwa Wananchi na kuchochea uwajibikaji.
"Licha kuandika Habari, makala na kuandaa Vipindi mbali mbali vinavyopiga chapuo uhuru wa Habari na maoni kwa Wananchi bado Waandishi Habari Pemba tunakabiliwa na changamoto mbali mbali kutoka kwa baadhi ya watendaji wa Serikali kama vile wa wakuu wa Mikoa, Wilaya, Jeshi la Polisi, Maafisa wadhamini hali inayotufanya tushindwe kutekeleza majukumu yetu ya kihabari ipaswavyo" Mhariri wa Gazeti la Zanzibar Leo Bakari Mussa





Comments
Post a Comment