Skip to main content

WAANDISHI WA HABARI VIJANA ZANZIBAR 'WASUKWA' KUZITAMBUA HABARI ZA UONGO.

NA, HASSAN MSELLEM – PEMBA

Waandishi wahabari wachanga Visiwani Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya kutambua taarifa sahihi katika kuelekea Uchanguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 29. 2025.

Akifungua mafunzo hayo kwa waandishi vijana kutoka Unguja na Pemba Mkurugenzi kutoka Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Mjini Unguja, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwandaa Waandishi Habari vijana kutekeleza majukumu ya kihabari kwa weledi katika Dunia ya sasa yaliyotawaliwa na matumzi mabaya ya ‘AKILI UNDE’ 

Aidha Mkurugenzi huyo amewasisitiza waandishi hao umuhimu wa kujifunza matumizi sahihi ya ‘AKILI UNDE’ katika kuhakikisha taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuelewa usahihi wake.

“Ngudu waandishi kama munavyofahamu kuwa katika dunia ya leo tumegubikwa na matumizi mazuri na mabaya Artificial Intelligence (AKILI UNDE) hivyo lengo la mafunzo haya kwenu ni kuona ni kwa namna gani mutaweza kutambua kati ya taarifa sahihi na zisizosahihi kupitia njia mbali mbali” Mkurugenzi kutoka Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania

Akiwasilisha mada juu ya namna ya kuzitambua taarifa za Uongo na Ukweli wa Kihistoria Mkufunzi wa masuala ya Digitali Ephraim Muchemi, amewataka waandishi hao kutumia programu mbali mbali kama vile Google lens, Google Earth nakadhalika ili ziweze kuwasaidia kupata ufafanuzi wa taarifa hizo.

“Kuna njia nyingi zinazoweza kuwasaidia katika kuzitambua taarifa za uongo na upotoshaji iwe maelezo, picha au hata video unaweza kuingiza sehemu ya maudhui hayo kwenye programu kama vile Google lens, Google Earth, True Caller nakdhalika na ukaweza kupata usahihi wa taarifa hizo” Mkufunzi wa masuala ya Digitali Ephraim Muchemi

Kwa upande wake, Afisa programu kutoka Muungano wa Klabu ya Waandishi Tanzania Andrew Marawiti, amewataka waandishi hao kuendelea kuyafanyia mafunzo kwa vitendo mafunzo hayo ili yaweze kuleta tija kwao na kwao na taifa kwa ujumla

“Kuwa kwenu hapa leo haikuwa Bahati mbaya tambueni kuwa mulikuwa wengi sana kwenye maombi ila nyinyi ndio tumeona munafaa zaidi kutokana na maelezo yenu kwenye maombi hivyo basi tunawaomba sana mukaendelee kuyatumia mafunzo haya kwa vitendo ili yaweze kuwajenga zaidi” amesisitiza

Akifunga mafunzo hayo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Abdalla Mfaume, amesema katika zama hizi za maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kumekuwa na ongezeko la ahabari za uongo na upotoshaji, hivyo amewaomba waandishi hao kuyafanyia kazi mafunzo hayo hususan katika kipindi hichi cha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.2025

“Katika kipindi hichi cha maendeleo ya sayansi na teknolojia changamoto za Habari za upotoshaji na uongo zimekuwa nyingi sana hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha munazitambua taarifa hizo ili zisiweze kuleta athari kwenu na taifa kwa ujumla” Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Abdalla Mfaume

Baadhi ya Waandishi hao wamepata nafasi ya kutoa neno ikiwemo kuushukuru Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kuendelea kuyafanyia kazi hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

"Kwanza nianze kwa kuwashukuru UTPC kwa mafunzo haya adhimu kwetu maana kwakweli mitandaoni hali sio shwari na sisi Waandishi ndio wahanga wa kubwa taarifa za uongo na upotoshaji kwa maana ya kutumia taarifa hizo" Salma Shaali Juma mwandishi kutoka Idara ya Uvuvi Zanzibar na Habari FM Radio 

Mafunzo hayo ya siku moja yalisyoshirikisha waandishi wa Habari Vijana kutoka Kisiwani Unguja na Pemba yameandaliwa na Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa ufadhili wa Netherlands (NL)

Mwiaba Kombo, Mwandishi wa Habari kutoka Radio Jamii Micheweni Pemba 
Salma Shaali Juma, Mwandishi wa Habari kutoka Idara ya uvuvi na Habari FM Radio.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...