Na, Fatma Muhammed Suleiman, Unguja Zulekha Ali Juma ni mama mwenye maono na dhamira ya kweli ya kutimiza ndoto zake. Alizaliwa mwaka 1971 visiwani Zanzibar, na safari yake ya elimu ilianza mwaka 1980 katika Skuli ya Haile Salasi Zanzibar, ambako alisoma darasa la kwanza hadi la nne. Aliendelea na masomo katika Skuli ya Konde, Micheweni Pemba, hadi kidato cha kwanza. Bi Zulekha alipendelea zaidi somo la siasa kwa sababu alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa, alipenda somo la historia na kujua asili ya nchi yake na maendeleo , na jiografia kwa shauku ya kutembelea maeneo mbalimbali. Akiwa skuli alikuwa kiongozi wa darasa ambapo pia alishiriki michezo mbalimbali. Alichagukliwa kuwa mwenyekiti wa chipukizi wa skuli na hatimae mwenyekiti wa chipukizi Mkoa wa Kaskazini Pemba. Ingawa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto zilizo nje ya uwezo wake, hakukata tamaa ya kutimiza malengo yake. Ndoto yake ilitimia rasmi mwaka 1993 alipojiunga na chama cha CUF ambapo alipata nafa...