Na, Hassan Msellem, Pemba
Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) imetoa takwimu za matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar katoka mwezi Agosti na Septemba 2025, ambapo jumla ya matukio 106 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa katika vituo mbali mbali vya Polisi huku Wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja kwa kuwa jumla ya matukio 17 sawa na asilimia 16.0
Akitoa takwimu hizo kwa waandishi wa Habari, waratibu wa madawati ya jinsia na wadau wengine Oktoba 22.2025 huko Gombani Pemba Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya mtakwimu Mkuu Zanzibar Sabina Raphael Daima, amesema jumla ya matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia 106 yameripotiwa mwezi Septemba 2025, ambapo waathirika wakubwa wakiwa ni watoto sawa asilimia 88.7 na wanawake wakiwa asilimia 11. 3
Aidha amesema kuwa miongoni mwa waathrika wa matukio hayo 94, wasichana 82 sawa asilimia 77.4 wavulana 12 sawa na asilimia 10.3
“Takwimu hizi zinaonesha matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar bado ni mengi na wahanga wakubwa wakiwa ni wanawake na watoto hivyo tuna jukumu kubwa la kila mmoja kusimama kwenye nafasi yake kupambana na makosa haya” amesema Mkurugrenzi huyo kutoka OCGS
Akiwasilisha mada katika utoaji wa takwimu hizo Mtakwimu kutoka Ofisi ya mtakwimu mkuu wa Serikali, Kitengo cha Jinsia na Ajira Asha Mussa, amesema watoto wenye umri kati ya miaka 15 hadi 17 ndio wahanga wakubwa wa matukio ukatili na udhalilishaji sawa na asilimia 54.3 ya matukio yote.
Ameongeza kuwa jumla ya majalada 85 yamepokelewa katika Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kwa mwezi Septembea ambapo wathumiwa wakuu wa wafanyaji wa matukio ya ukatili na udhalilishaji ni wapenzi matukio 38, watu wasiojuilikana matukio 28, majirani matukio 22, watu wengine matukio 17 na baba mdogo tukio moja
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Tawkimu Jinsia na Ajira Fahima Mohammed Mussa, amewataka wadau hao kuandaa vipindi na mikakati itakayosaidia kupunguza idadi ya matukio hayo katika jamii.
Idadi ya matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa Wilaya zote za Unguja na Pemba kwa mwezi September 2025, ni kama ifuatavyo
WILAYA YA MATUKIO
Magharib ‘B’
Matukio 17
Magharaib ‘A’
Matukio 16
Kaskazini 'A'
Tukio 1
Kaskazini ‘B’
Matukio 13
Wilaya ya Kati
Matukio 15
Wilaya ya Kusini
Matukio 8
Wilaya ya Chake Chake
Matukio 9
Wilaya ya Mkoani
Matukio 6
Wilaya ya Wete
Matukio 5
Wilaya ya Micheweni
Matukio 2
Lengo la kuu la takwimu hizi za matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia ni kutoa msaada kwa watunga Sera, waandishi wa habari na wanahakati ili Sera na kazi juu ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia zenye kuendana na hali halisi ya tatizo hilo.
.jpeg)




Comments
Post a Comment