Skip to main content

PENYE NIA PANA NJIA: SAFARI YA KISIASA YA ZULEKHA ALI JUMA.

Na, Fatma Muhammed Suleiman, Unguja 

Zulekha Ali Juma ni mama mwenye maono na dhamira ya kweli ya kutimiza ndoto zake. Alizaliwa mwaka 1971 visiwani Zanzibar, na safari yake ya elimu ilianza mwaka 1980 katika Skuli ya Haile Salasi Zanzibar, ambako

alisoma darasa la kwanza hadi la nne. Aliendelea na masomo katika Skuli ya Konde, Micheweni Pemba, hadi kidato cha kwanza.

Bi Zulekha alipendelea zaidi somo la siasa kwa sababu alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa, alipenda somo la historia na kujua asili ya nchi yake na maendeleo , na jiografia kwa shauku ya kutembelea maeneo mbalimbali.

Akiwa skuli alikuwa kiongozi wa darasa ambapo pia alishiriki michezo mbalimbali. Alichagukliwa kuwa mwenyekiti wa chipukizi wa skuli na hatimae mwenyekiti wa chipukizi Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Ingawa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto zilizo nje ya uwezo wake, hakukata tamaa ya kutimiza malengo yake.

Ndoto yake ilitimia rasmi mwaka 1993 alipojiunga na chama cha CUF ambapo alipata nafasi ya mshika fedha wa tawi la Sebleni Amani, Wilaya ya Mjini Unguja, na baadaye kuwa wakala wa waandikishaji na wapiga kura.

Mwaka 2010 aligombea ubunge Jimbo la Kwahani. Ingawa hakupata ushindi lakini hakuka tamaa na aliendelea kushiriki kwenye kamati ya uongozi wa jimbo na kuwa Katibu wa Wanawake Jimbo la Kwahani. Nafasi hiyo aliihudumia kwa bidii ambapo na kuchukua tena fomu ya kugombea ubunge mwaka 2025.

Kwa Bi Zulekha, siasa siyo tu ndoto binafsi, bali ni njia ya kupigania maendeleo.

“Mazingira yaliyonizunguka yanahitaji mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Nikaona kwanini nisiwe mwanamke atakayeleta maendeleo kwa wanawake wenzangu na wenye uhitaji maalumu kwa kuwapa kipaumbele,” alisema.

Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC, 2020), ni asilimia 23 pekee ya wagombea wa nafasi za ubunge na uwakilishi walikuwa wanawake.

Ni katika mazingira haya ndipo Bi Zulekha anaendeleza mapambano yake ya kisiasa kwa ujasiri na msimamo thabiti.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar (OCGS, 2022), zaidi ya asilimia 60 ya wanawake wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo hufanya hivyo kupitia vikundi vya ushirika au vikoba.

 Hili limemtia nguvu Bi Zulekha kwa kufanikiwa kuwawezesha wanawake kiuchumi, kifikra na kimaadili kupitia vikundi vya kijamii kama ZamZam na vingine katika Shehia ya Sebleni.

Umoja ni nguvu, Bi Zulekha anaamini kuwa maendeleo ya wanawake hayawezi kuletwa na mtu mwingine, bali na wanawake wenyewe kupitia mshikamano na mashirikiano.

 “Maendeleo ya wanawake huletwa na wanawake wenyewe kwa kusaidiana kwa hali na mali na kuwa na umoja ili kufikia malengo yetu,” anasema.

Kupitia jitihada zake zimewawezesha wanawake wa Sebleni kupata mitaji na mafunzo ya ujasiriamali.

Na hii inaakisi ile methali ya chanda chema huvikwa pete kwani KUTAIBA Succos ilimtunukia cheti cha heshima kwa jitihada hizo. Aidha, mafunzo ya uongozi wa siasa kutoka TAMWA, yalimuongezea ujasiri Zaidi wa kuendelea na harakati zake.

Maneno si mkuki, safari yake ya uongozi ilikumbana na changamoto ya kubezwa na kudharauliwa kwani wapo waliompiga madongo wakisema

“Wameshindwa wanaume, sasa nyie wanawake mtaweza nini?”

Kauli kama hizo zilimpa msukumo zaidi wa kuthibitisha kuwa mwanamke anaweza. Kwa Bi Zulekha walizidisha mafuta katika moto.

Ripoti ya UN Women (2023) inabainisha kuwa changamoto ya rasilimali fedha ni kikwazo kwa wanawake wengi wenye nia ya kuingia katika uongozi. Hili lilimkumba Bi Zulekha ambapo alilazimika kutumia nguvu binafsi za nyumba kwa nyumba ili kutimiza lengo lake.

Watoto wake pia nao walimpa wakati mgumu kuingia kwenye siasa kwa hofu ya changamoto angeliweza kukutana nazo. Busara na hekima zake zililainisha mioyo. Hii ilichangiwa zaid na mumewe Bwana Hamad Khamis Hamad ambae alimuunga mkono mkewake kwa shauku ya kuona lengo lake linatimia. 

Bwana Hamad ambae alijaaliwa watoto saba na Bi Zulekha alifanikiwa kuwaelimisha wale waliokuwa na mashaka naye na kuendelea na harakati zake hadi leo.

Nasra Hamad Khamis, mmoja wa wao anaeleza kuwa anajivunia kuwa na mama mwenye upendo, anayeshirikiana na watu wote bila ubaguzi.

“Ameonyesha mfano kuwa mwanamke anaweza kushika nafasi za uongozi wa kisiasa na kijamii.” Alisema Nasra kwa furaha.

Katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi za uongozi kwa kupitia uchaguzi mkuu 2025, wagombea wanawake wanamshukuru kwa jitihada zake za kuwashika mkono 

“Bi Zulekha kuwa ni mpenda mashirikiano, Hata kwenye changamoto yeye hutupa matumaini na kutufanya tushinde”. Alisema Mwanayasini Mustafa Vuai, mgombea udiwani wa Jimbo la Kwahani kupitia ACT Wazalendo.

Naye Sharifa Mohamed Alawi, mgombea uwakilishi wa jimbo hilo, anaeleza:

“Bi Zulekha ni mtu wa watu na mcheshi ameonyesha mfano wa uongozi na kujituma kwa maendeleo ya wanawake.”

Safari ya Bi Zulekha Ali Juma ni kielelezo cha mwanamke jasiri anayesimama kwa imani, maadili na juhudi binafsi. Anaamini kuwa mabadiliko yanawezekana kupitia siasa, mshikamano wa kijamii na nguvu ya wanawake.

 “Penye nia pana njia,” anasisitiza Bi Zulekha kauli inayob

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...