MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA
Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho.
“Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema
Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo.
Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafasi ambayo amesema haikuwa rahisi kuipata na kuweza kuitumikia ipaswavyo lakini kutokana uzoefu na umahiri wake katika siasa na uongozi amekuwa kiongozi wa mfano katika chama chake cha ADC.
Ameongeza kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.2025 alitamani kugombea nafasi ya Ubunge lakini kutokana na majukumu alionayo ya kiongozi ameshindwa kugombea nafasi hiyo na kutoa wito kwa wanawake wenzake waliogombea nafasi za uongozi kuwa sera mzuri zitakazowagusa wananchi na zinazoweza kuetekelezeka
Amesema “Nilitamani na mara hii nigombee nafasi ya ubunge wa kuchaguliwa badala ya Viti Maalumu lakini kutoakana na majukumu mengi nilionayo nilikhofia kukosa muda wa kuwasimamia wagombea wangu kwasababu mimi ndio kiongozi kwa Pemba” Kamishna wa ADC kanda ya Pemba Mariam Muhene,
Katibu mkuu taifa wa Chama cha ADC Mwalimu Hamad Aziz, amesema miongoni mwa viongozi wa chama cha ADC ambao fikra zake zinasaidia kukijenga chama hicho ni pamoja na Bi. Mariam Muhene kwani ana nguvu ya ushawishi, muadilifu na anaependa haki na sawa ndani nan je ya chama pamoja na kutoa msaada kwa watu wa makundi maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu
Ameongeza kuwa kutokana na fikra na maono yake amefanikiwa kuanzisha mfumo wa kikoba kwa wanawake wa chama hicho ambacho kinawasaidia katika shughuli zao mbali mbali zikiwemo za kiuchumi na siasa
“Mariam Muhene ni mwanamke jasiri anajitoa ana uwezo wa kushawishi mtu hana haya kwenye haki, uadilifu na usawa kwenye jamii ni mwanamke aliyejipambanua kisiasa” Katibu mkuu taifa wa Chama cha ADC Mwalimu Hamad Aziz
Abdul-hamid Said Hamad ni mwanachama wa chama cha ADC, amesema Bi. Mariam ni mwanamke nguli wa kwenye hasa za upinzani kutoka mwaka 1992, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini na ameweza kudumu kwenye siasa mpaka sasa licha ya dhoruba kadhaa alizokutana nazo
Mwanachama huyo ameongeza kuwa Mariam amekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake wengi kutoakana na ushupavu wake kiutendaji ikiwemo utatuzi wa migogoro ndani na nje ya chama
Amesema “tukumbuke siasa imebeba mambo mengi sana ikiwemo ushindani, migogoro ya ndani ya chama na nje kama tunavyoshuhudia lakini licha changamoto zote zilizojitokeza Mariam hakukata tamaa akasema siasa basi bado anasimama na kusonga mbele”
Mkurugenzi wa Jumuiya utetezi wa Kijinsi na Mazingira Pemba (PEGAO) Hafidh Abdi Said, amesema Mariam Muhene ni miongoni mwa wanawake 2054 waliopatiwa mafunzo Kisiwani Pemba kupitia mradi wa uhamasishaji wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi (SWIL) ambao walipatiwa mafunzo mbali mbali yaliyowawezesha kuwa vinara katika siasa na uongozi
“Bi. Mariam ni miongoni mwa matunda ya mradi wa SWIL ulioaza mwaka 2020 ambapo zaidi ya wanawake 2000 Kisiwani Pemba walipata mafunzo kupitia mradi huo na wengi wao leo ndio wamekuwa wanawake wakupigiwa mfano kwenye masuala ya siasa na uongozi” amesema
Sakina Haji Mbarouk ni jirani wa Mariam na mgombea wa nafasi ya Uwakilishi jimbo la Micheweni kupitia chama cha Ukombizi wa Umma (CHAUMA) amesema miongoni mambo aliojifunza kutoka kwa Mariam Muhene ni pamoja na mashirikiano kwa wanawake wenzake yake bila ya kuangalia hali wala itikadi ya chama, hivyo jirani huyo amewaomba wanachama wa ADC na wananchi kwa ujumla kumuunga mkono Mariam endapo atagombea nafsi ya uongozi ili aweze kuwaletea maendeleo
“Mimi ni mwanachama wa CHAUMA na Bi. Mariam ni mwanachama wa ADC lakini hatujawahi kukwazana hata siku moja na ni mara kadhaa ameshawahi kunipa ushauri kuhusu mambo mbali mbali ndie alinipa ushawishi na hamasa ya kugombea nafasi ya Uwakilishi katika chama changu” jirani
Adil Mmaka Abdalla ni mtoto wa nne kwenye familia ya Bi. Mariam na Bwana Mmaka Abdalla, amesema licha ya mama yake kujishughulisha na siasa tangu yeye akiwa na umri mdogo lakini wamepata matunzo na malezi bora yaliyochangia kupata elimu ya dini na dunia, pamoja na kuwalea katika mazingira ya ujasiri na kujiamini
“Alianza kuingia kwenye siasa tangu mimi nikiwa mdogo miaka ya 1995 kupitia chama cha CUF lakini ametulea vizuri na sijawahi kushuhdia mgogoro wowote kati yake na baba hakika mama ni mwanamke anaependa haki, usawa na jasiri mno” amesema Adil Mmaka Abdalla, mtoto wa Mariam Muhene

Comments
Post a Comment