HASSAN MSELLEM, PEMBA
Abdalla Rashid Hassan (Mgunya) mwenye umri wa miaka 30 mkaazi wa Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba amehukumiwa kwenda chuo cha mafunzo (JELA) kwa muda wa miaka 30 kwa Kutenda makosa nane ya udhalilishaji yakiwemo ya kutorosha, shambulio la aibu na kubaka.
MAKOSA MATANO YA KUTOROSHA
Mbele ya hakimu wa mahakama ya kupambana na makosa ya udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake Taki Abdalla Habib imeelezwa na mwendesha mashtaka Othman Mzori kuwa tarehe 3\01\2025 saa 8:30 za mchana huko bonde la Mjananza Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba mshtakiwa aliwachukua watoto watano wenye umri kati ya miaka 7, 9, 11, 12 na kuwapeleka maporini katika bonde la Sinanga Ziwani, jambo ambalo ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 113 kifungu kidogo cha kwanza (a) Sheria nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar.
KOSA LA SITA
Shambulio la kawaida
Tarehe 3\01\2025 saa 9:25 za jioni huko Sininga Ziwani Wilaya ya Chakwe Chake Mkoa wa Kusini Pemba alimshambulia kwa kumpiga bakora sehemu mbali mbali za mwili wake watoto wakike mwenye umri wa miaka 11 kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake jambo ambalo ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 229 cha Sheria nambari 6/2018 Sheria ya Zanzibar.
KOSA LA SABA
Shambulio la aibu
Kinyume na kifungu 114 kifungu kidogo cha 1 Sheria nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar, mnamo tarehe 3\01\2025 saa 9:30 za jioni huko bonde la Sininga Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba bila ya halali na kwa njia ya aibu alimvua nguo mtoto wakike mwenye umri wa miaka 11 na kumshambulia kwa kumchezea sehemu ya kifuani na kumtia mikono katika sehemu yake ya siri ya mbele.
KATIKA KOSA LA NANE
Kubaka
Kinyume na kifungu cha 108 kifungu kidogo cha 1 kifungu kidogo cha 2 kifungu kidogo cha i na kifungu cha 109 na kifungu kidogo cha 1 cha Sheria nambari 6.2018 Sheria ya Zanzibar, tarehe 3/01/2025 saa 9:35 za jioni katika bonde la Sininga Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba alimbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12.
Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilisomwa 11/02/2025 na jumla ya mashahidi saba walitoa Ushahidi wao mahakamani hapo Ushahidi uliouwezesha mahakama kumtia hatiani na kuamuru kwenda chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 106 kwa makosa yote 8 adhabu hizo ziende sambamba hivyo atatakiwa kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 30.
Ikumbukwe kuwa Oktoba 22.2025 mwandishi wa Habari hizi aliripoti taarifa ya Hakimu Said Hakimu mwenye umri wa miaka 36 mkaazi wa Jondeni Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba kuhukumiwa kutumikia chuo cha mafunzo miaka thelathini (30) kwa kosa la kumbaka mtoto wakike mwenye umri wa miaka 7 kwa mujibu wa hati ya mahakama ingawa wazazi wake walisema ana umri wa miaka nne.
Kwa mujibu wa Takwimu za matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia zilizotolewa na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwenye Ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani Pemba Oktoba 22.2025 zinaeleza jumla ya matukio 106 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa katika mwezi Septemba, 2025 ambapo waathirika wengi wakiwa ni watoto sawa asilimia 88.7 ni wanawake na 11.3 wanaume. Miongoni mwa waathirika watoto 94, wasichana wakiwa 82 sawa na asilimia 77.4 na wavulana ni 12 sawa na asilimia 10.3
Aidha takwimu hizo zimeeleza idadi ya matukio ya ubakaji kwa mwezi huo wa Septemba Zanzibar yalikuwa ni 57, waathirika 54 ni wasichana, kulawiti matukio 11, kuingilia kinyume na maumbile matukio 5, kutosha 15. Kuingilia maharimu 1 na kutoa mimba tukio moja (1).
.jpeg)
Comments
Post a Comment