Skip to main content

Rushwa ya ngono, ukosefu wa fedha vikwazo kwa Wanawake kutimiza ndoto zao za kuwa Viongozi

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA


KATIBA ZA VYAMA

Katiba za vyama vingi vya Siasa nchini zimezingatia usawa wa Kijinsia katika Uongozi ndani na nje ili kuwepo kwa usawa katika vyama hivyo. Katiba ya Chama cha Mapinduzi CCM, Sura ya Pili Fungu la Pili ibara ya 16 inasema “Kiongozi wa CCM ni kila Mwanachama mwenye dhamana yoyote katika CCM aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba. Ibara ya 17 inaeleza sifa za kiongozi ni pamoja na kutosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa. 

Katiba ya Chama cha Alliance for Change and Transparency - ACT Wazalendo SEHEMU YA PILI, imeeleza Sifa za kuwa kiongozi katika Chama hicho ikiwemo “kuwa na mwenendo mzuri na Maadili ya Viongozi” Lakini licha ya haki ya Usawa wa Kijinsia iliyotolewa na Katiba za vyama Siasa bado Wanawake wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha kuanzia fedha za kuchulia fomu pamoja na kampeni, hali inayosababisha Wanawake wengi kushindwa njia kugombea nafasi za Uongozi kupitia vyama vyao.

WANAWAKE WALIOWAHI KUGOMBEA

Mgombea wa nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mwamize Mohammed, amesema bado wanawake wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwe ukosefu wa fedha, ubaguzi wa kijinsia pamoja na rushwa ya ngono hali inayosababisha wanawake wengi kukosa fursa za kuwa viongozi.

Asema “Bado wanawake tunakabiliwa na changamoto lukuki katika kugombea nafasi za Uongozi kwasababu kama huna fedha za kuwapa wajumbe kwa sera tupu za maneno huwezi kuzingatiwa, kuna changamoto ya rushwa ya ngono binafsi nimekumbana nayo ila nimefanikiwa kuikwepa lakini pia kudharaulika chakusikitisha zaidi wanawake wenzetu ndio vinara wa kuwashawishi wanachama wasituchague” 

Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Wawi Hadija Anuwar Mohammed, amesema licha ya Chama hicho kuwa na Sera ya Usawa wa Kijinsia lakini bado Wanawake wamekuwa wakikabiliwa na khofu ya kugombea nafasi za Uongozi kutokana na dhana potofu kuwa mwanamke hawezi kuwa na uwezo wa kufanya vizuri katika nafasi za uongozi

“Tatizo sio muamko wala kujiamini lakini tatizo wanaume wakikusikia tu kuwa unataka kugombea nafasi ya Jimbo wanakufata na kukushawishi na kukutia khofu kwamba kwanini usigombania nafasi za UWT sasa hiyo ndio inatufanya wanawake kuwa na khofu ya kugombania nafasi za Jimbo ila kwakweli wanawake tuna uwezo mzuri kuliko hao wanaume” Maoni ya Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Wawi Hadija Anuwar Mohammed

WADAU WA USAWA WA KIJINSIA 

Wadau na watetezi wa Usawa kijinsia walisema tatizo la ukosefu wa fedha za kampeni na umashuhuri ni miongoni mwa vikwazo vikuu vinavyowafanya wanawake washindwe kutimiza ndoto zao za kuwa viongozi na badala yake ni wanawake wachache tu wanaohimili mchakato huo.

“Sasa hivi wanawake wameamka sana tukilinganisha na miaka ya nyuma na hii inatokana na elimu na hamasa ambazo tumekuwa tukizitoa kwa muda mrefu Imani yetu Imani yetu ile Sera ya 50 kwa 50 itafanikiwa ifikapo 2030 endapo changamoto zinazowakabili zikipatiwa ufumbuzi” Omar Saleh Mwanamme wa Mabadiliko kutoka Shehia ya Kilindi

JUMUIYA ZA UTETEZI WA HAKI ZA WANAWAKE

Mratibu wa Jumuiya ya Utetezi wa Kijinsi na Mazingira Pemba (PEGAO) Dina Juma Makota, amesema licha ya wanawake wengi kuhamasika kujiunga na vyama vya siasa na kugombea nafasi za uongozi lakini bado wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa fedha, mfume dume na rushwa ya ngono hali inayochangia kuzima ndoto zao.

“Niwaombe wanawake wote wanaopitia changamoto za ubaguzi, unyanyasaji na kudaiwa rushwa ya ngono na fedha kujiamini na kuziripoti changamoto hizo kwa vyombo husika au kwa wadau wa utetezi wa haki za wanawake ili zipatiwe ufumbuzi na sio kuzikalia kimya lakini pia viongozi wa vyama wanatakiwa kubadilika na kuwaamini wanawake kuwa ni viongozi wazuri, mfano mzuri ni Rais Samia kumteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Katibu Mkuu wa CCM na Waziri wa Ulinzi Mhe. Stagomena Tax na wanafanya vizuri” Mratibu wa Jumuiya ya Utetezi wa Kijinsi na Mazingira Pemba (PEGAO) Dina Juma Makota.

Kaimu Mratibu wa Tamwa Pemba Amina Ahmed, amesema katika kuwasaidia Wanawake wanaokabiliwa na changamoto kipindi cha kampeni na uchaguzi ni kuanzisha Mtandao wa kutoa za Taarifa Za Mapema (Early Worning Network) ili waweze kutoa taarifa za changamoto zinazojitokeza dhidi yao. 

“Ssi tukiwa taasisi tunayopaza sauti za wanawake tunazipokea changamoto zote zinazowakabili wanawake wakati huu wa kampeni na kabla ya Uchaguzi tumeanzisha mtandano wa Mfumo wa Taarifa za Awali (Early Worning Network) mtandao unawapa fursa wanawake kupaza sauti zao dhidi ya viashiria vyote vinavyoweza kuwarudisha nyuma katika mchakato wa kugombea, kampeni na kipindi cha Uchaguzi” amefafanua

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

Makamo Mwenyekiti Mkutano Mkuu Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Mkunga Hamad Sadala, alisema chama cha ACT Wazalendo ni Chama cha kwanza kuanzisha Sera jinsia lengo likiwa ni kuweka usawa katika chama hicho pamoja na kutambua uwezo na nguvu ya wanawake katika ujenzi wa Taifa.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema mkakati wa chama cha ACT Wazalendo ni kuwachukulia hatua kali Viongozi na wagombea watakaobainika kutenda vitendo vya ubadhirifu ikiwemo rushwa ataondolewa katika nafasi anayogombea ili iwe fundisho kwake na wagombea wengine.

“Miongoni mwa mikakati yetu Chama cha ACT Wazalendo katika kudhibiti vitendo vya ubadhirifu ikiwemo rushwa, ubaguzi na kadhalika ni kwamba mgombea yeyote atakaebainika kutenda makosa hayo hata kama ameshinda kwa kura zote hatokuwa tena mgombea wa nafasi hiyo hii itakuwa funzo kwake na kwa wagombea wengine” alisema 

Mariam Mohammed Muhene Kamshna Kanda ya Pemba Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) amesema Chama cha ADC kinazingatia usawa wa Kijinsia na watu wenye mahitaji maalum katika ngazi zote za Uongozi bila ya kuangalia jinsia, rangi wala hali ya mwanachama hali inayochangia idadi kubwa ya viongozi Wanawake katika Chama hicho.

Amesema “Chama chetu ndio chama pekee ambacho kinazingatia jinsia lakini sio jinsia tu bali makundi ya watu wenye mahitaji maalum na hili linadhihirika kwa mifano mbali mbali kwa mfano Naibu Katibu Mkuu wa Chama ni Mwanamke na Makamo mwenyekiti pia ni mwanake lakini katika Baraza Kuu la Uongozi ni 50 kwa 50 hii yote inamaanisha kuwa Chama cha ADC ni chama kinachozingatia zaidi usawa wa Kijinsia kwahivyo katika chama chetu hakuna masuala ya kuwanyanyasa wanawake kwasababu nalisimiamia vizuri hilo ila tu changamoto inayotukabili ni ukosefu wa fedha kwasabau hatuna ruzuku” 

Mwisho.


Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...