Makala Na, Hassan Msellem
Katika uzinduzi wa programu ya kuinua haki za watu wenye ulemavu ya CADir (Collective Action for Disability Rights) katika kutatua changamoto za watu wenye ulemavu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetaja hatua inayochukua katika kuimarisha ushiriki wao katika ngazi za uamuzi kutoka asilimia 2% hadi 5% ifikapo mwaka 20230.
Utambuzi wa watu wenye ulemavu katika azimio la Arusha la mwaka 1967, kuwa miongoni mwa makundi machache yanastahili usaidizi kutoka kila sekta ikiwemo jamii, elimu, ajira na Uongozi ili kuhuisha haki na ustawi wa watu wenye ulemavu nchini.
Wanawake wenye Ulemavu kupitia vyama mbali mbali vya siasa wameomba kupunguziwa kiasi cha kulipia fomu za kugombea nafasi za uongozi ili waweze kushiriki katika haki hiyo.
Wakizungumza na Pemba Post Blog kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake wenye ulemavu wamesema gharama za fomu za kugombea nafasi za kisiasa kama vile Uwakilishi, Ubunge na Uraisi ni kubwa hali inayochangia baadhi yao kushindwa kuhimili gharama hizo.
Mgombea wa Viti Maalum (UWT) kutoka Chama cha Mapinduzi CCM Bi. Awena Rashid, amesema kiasi cha shilingi laki tano kwa wanawake wa kawaida na wenye ulemavu ni kubwa sambamba na utaratibu wa kutakiwa kwenda Dodoma kujadiliwa kwa gharama zao binafsi hali inayowasabaishia usumbufu na mzigo wa gharama
“Kwakweli laki tano kwa mwananchi wa kawaida tena mwenye ulemavu ni kiasi kikubwa mno kwanini wasiweke kiasi ambacho kitakuwa nafuu kwa watu wote na haishii hapo tunatakiwa kwenda Dodoma katika mchakato wa kujadiliwa wakati tumetuma CV zetu ikizingatiwa ghamaza zote ni juu yetu” mgombea wa UWT Mkoa wa Kaskazini Pemba Bi. Awena Rashid
Katija Mbarouk Ali mgombea wa nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Kojani, amesema gharama ya fomu ya kugombea nafasi ya Uwakilishi kutoka shilingi laki moja mwaka 2020 hadi laki tano 2025 ni gharama kubwa ambayo imemlazimu kutumia nguvu za ziada kuihimili kiasi ambacho angeweza kukukitumia kwenye harakati nyengine za kimaisha
Katija ameongeza kuwa kiwango hicho kinanyima fursa kwa wanawake hasa wenye ulemavu kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ambayo ni haki yao ya msingi
“Uchaguzi wa mwaka 2020 fomu ilikuwa ni shilingi laki moja lakini lakini mwaka huu 2025 fomu ilikuwa shilingi laki tano mwanamke kama mimi mwenye ulemavu ambaye sina kazi maalumu ya kufanya napataje kiasi hicho” amesema
Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) Hidaya Mjaka Ali, amesema kiasi hicho cha fedha za fomu zinachangia wanawake wengi hasa wenye ulemavu kushindwa kuhimili gharama hiyo hivyo ameviomba vyama vya siasa nchini kuwapunguzia watu wenye ulemavu gharama hizo ili waweze kushiriki siasa bila ya vikwazo.Mwenyekiti wa Jumuiya watu wasiona Zanzibar Kisiwani Pemba (ZANAB) Mansour Nassor, amekiri kupokea kupokea kesi kadhaa kutoka kwa wanawake wenye ulemavu wa macho ambao wamelalamikia kukosa haki ya kugombea kutokana na ukosefu wa fedha za fomu na kampeni
“Sio mara moja wa mbili kila uchaguzi napokea malalamiko kutoka kwa wanachama wangu hasa wanawake wanaotia nia ya kugombea nafasi za uongozi kuwa fedha ya fomu ni kubwa mno hawana uwezo nayo na hata wakijikusuru kupata pesa ya fomu hawana pesa za kufanyia kampeni” amesema Mwenyekiti huyo
Kamishna wa Chama cha ADC Kanda ya Pemba Mariam Mohammed Muhene, amesema chama cha ADC ni chama cha kwanza kinachozingatia makundi maalumu yakiwemo watu wenye Ulemavu ili nao waweze kupata haki yao ya kushiriki katika siasa na uongozi, hivyo amevitaka vyama vyengine vya kisiasa kulizingatia kundi hilo hasa wanawake
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Utetezi wa Kijinsia na Mazingira Pemba (PEGAO) Hafidh Abdi Said, amesema wakati umefika kwa vyama vya siasa kutambua mchango wa wanawake wenye ulemavu katika siasa na uongozi ili nao wawezekapata haki yao ya kuwa viongozi.
Amesema “mwanzo tulikuwa tunawasemea sana wanawake kwa ujumla lakini sasa kuna haja ya kuwasemea wanawake wenye ulemavu kwasababu Kundi hilo linahitaji uangalizi wa ziada ili kuhakikisha wanashiriki ipaswavyo katika mausala ya siasa na uongozi”




Comments
Post a Comment