Skip to main content

'Ongezeko la viongozi wanawake kwenye vyombo vya maamuzi, chachu ya maendeleo Zanzibar.

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM- PEMBA

 Ni miaka mingi sana vyombo vya maamuzi nchini Tanzania vimekuwa vimehodhiwa na wanaume kwa asilimia kubwa kutokana na wanawake kukosa muamko na kunyimwa fursa ya kugombea nafasi za uongozi katika vyama vyao vya siasa licha ya kuwa wao ndio wafuasi wakubwa wa vyama hivyo.

Lakini kuanzishwa kwa miradi mbali mbali yenye lengo la kuwawezesha wanawake kushiriki katika haki yao ya siasa na uongozi ikiwemo mradi wa uhamasishaji wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi (SWIL) kumeongeza muamko na hamasa ya wanawake kujiunga na vyama vya siasa pamoja na kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kama vile udiwani, uwakilishi, ubunge na hata uraisi.

Hilo linadhihiri kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29.2025 ambapo kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa habari Tanzania Tamwa, Zanzibar Agosti 20.2025 imeeleza kuwa jumla ya wanawake 13 nchini kutoka vyama mbali mbali vya siasa wamegombea nafasi ya uraisi na umakamu wa raisi idadi ambayo ni sawa asilimia 36 kati ya wagombea wote waliochukua fomu kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambao idadi yao ni 36 idadi ambayo inaonesha kupanda ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2020 ambapo kati ya wagombea 30 wa nafasi ya uraisi na umakamu wa raisi, wanawake walikuwa 7 pekee saw ana asilimia 23.3 kati ya hao watano (5) walitoka Zanzibar.

Mkataba wa kutokomeza aina zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake wa mwaka 1979 (CEDAW) na Umoja wa Africa, 2023 (AU) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, 2008 na 2015 (SADC) umesema hatua hii itawatia moyo zaidi wanawake na watoto wa wakike kutimiza ndoto zao za kuwa viongozi bila ya vikwazo vyovyote.

Maoni ya wananchi wengi hasa wanaume linapokuja suala la wanawake kuwa viongozi huleta sura tofauti lakini baada ya wadau wa usawa wa kijinsia kutoa hiyo kwasasa suala hilo linaonekana ni lakawaida na linaungwa mkono na wananchi wengi hata wale waliokuwa wanadhani suala la wanawake na uongozi ni kinyume na miongozo ya dini, mila na utamadaduni.

Salum Juma Ali, mkaazi wa Wambaa Wilaya ya Mkoani Pemba, amesema “Kwakweli inafurahisha sana kuona dada zetu na mama zetu wameanza kuamka na kuona suala la uongozi ni haki yao ya msingi kwa kupata muamko wa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ili kwenda kuwawakilisha wanawake wenzao na wananchi kwa ujumla”

Nachia Ali Jamal, mgombea wa Viti Maalum ngome ya chama cha ACT Wazalendo ameanza kuzishukuru taasisi zilizomuwezesha kupata elimu na uthubu wa kuwa mwanachama imara katika chama chake na kuthubu kugombea nafsi mbali mbali huku akiahidi kwenda kuwawakilisha wanawake wenzake endapo atapata fursa ya kushika nafasi hiyo

“Kwanza nianze kwa kuwashuru wadau wetu wakubwa wa masuala ya wanawake na uongozi ambao Tamwa na Pegao kwa elimu na muamko waliotupatia wanawake” amesema

Aidha ameitaka tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) na tume huru ya uchaguzi Tanzania (INEC) kutenda haki kwa kuwatangaza washindi kutokana na kura walizopata ili kuongeza idadi ya wanawake katika vyombo vya maamuzi.

“nichukue nafasi kuziomba tume zetu za uchaguzi INEC na ZEC kutenda haki bila ya kuangalia chama wala jinsia ili kila ambaye ameshinda kwa mujibu wa kura apate haki yake hii itaepusha fujo na vurugu ambapo yakitokea hayo waathirka wakuu ni wanawake na watoto” 

Mwenyekiti wa Chama cha ukombozi wa umma (CHAUMA) Mkoa Kusini Pemba Mariam Saleh Juma, amesema kuongezeka kwa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi kutasaidia kupatikana kwa haki za wanawake nchini kwani wanawake watapata fursa ya kueleza changamoto zo.

Amesema “Kwangu hii naiona ni fursa muhimu sana kwani muda mrefu wanawake hatukuwa tunapata nafasi za kugombea kama ilivyo sasa hivyo tutapa nafasi ya kueleza changamoto, mafanikio lakini kutoa ushawishi kwa wanawake wengine”

Mratibu wa Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba (TUJIPE) Tatu Abdalla Msellem, amesema endapo wanawake watapata ridhaa ya kuingia kwenye vyombo vya maamuzi wataweza kusaidia taifa litapiga hatua kubwa kimaendeleo kutokana na uaminifu walionao pamoja utendaji kama inavyodhirika kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan

“Ni jambo la faraja na kujivunia sana kuona muda na nguvu kubwa tuliotumia kuwaelimisha na kuwahamasisha wanawake kushiriki katika siasa na uongozi sasa matunda yanaonekana idadi ya wanawake waliojitokeza kugombea nafasi mbali mbali” Tatu Abdalla Msellem, mratibu TUJIPE 

Ameongoza kuwa licha hatua hiyo bado wapo baadhi ya wananchi hasa wanaume wenye dhana kuwa mwanamke hana haki ya kuwa kiongozi dhana ambayo wanawake watakaopata fursa ya kuwa viongozi wanapaswa kuifuta kwa vitendo

“lakini dhana ya mwanamke kuwa hawezi kuwa kiongozi kama mwanaume bado ipo na haiwezi kufutika kirahisi kwasababu mfumo tuliotoka nao ni mfume dume ila mbona tunayo mifano mizuri ya wanawake wanaofanya vizuri kuliko wanaume”

Mwanaume wa mabadiliko Shaabani Juma Kassim, amesema suala la kuongezeka kwa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi kutawawezesha wanawake kujiimarisha kisiasa na kiuchumi pamoja na kutoa hamasa na ushawishi kwa wanawake wengine ambao wana ndoto za kuwa viongozi 

“hili jambo ni jema sana kwasababu wanawake watajiwezesha kiuchumi lakini pia kutoa mawazo ambayo yanawagusa wanawake moja kwa moja badala ya Mawazo hayo kutolewa na wanaume” Shaabani Juma Kassim

Ameongeza kuwa ongezeko hilo limechangiwa na juhudi kubwa zilizofanywa na wadau mbali mbali zikiwemo asasi za kiraia, wanaharakati pamoja na wahisani kutoka mataifa mbali mbali katika kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki na fursa sawa ya kushiriki kwenye siasa, uongozi na uchumi.

“Lakini ifahamike kuwa mafanikio haya hayakuja tuk ama mvua kuna kazi kubwa imefanywa na wadau wakiwemo taasisi ya tamwa, Pegao, Tujipe, Zafela, wanaharakati pamoja wahisani kutoka mataifa mbali mbali kama vile Ubalozi wa Norway nchini Tanzania” amesema

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...