Skip to main content

Elimu ya Uongozi Nguzo Muhimu kwa Mwanamke Katika Uongozi

 Makala Na Fatma M. Suleiman

Mitazamo kuhusu nafasi ya mwanamke katika uongozi imeendelea kubadilika taratibu. Wapo wanaoamini kwamba mila na desturi haziruhusu mwanamke kuwa kiongozi, wengine wanaona hakuna pingamizi la kimaadili wala kidini linalozuia mwanamke kushika nafasi za juu za maamuzi.

 Bikame Sheha Ussi, Mkuu wa Divisheni ya Pensheni Jamii na Maendeleo ya Wazee, anabainisha kuwa historia za dini pia zinaonyesha wazi kwamba wanawake hawajazuiwa kuwa viongozi. 

 “Kwa upande wa Dini ya kiislamu haijakataza mwanamke kuwa kiongozi, bali inasisitiza kuzingatia mipaka na maadili.”

Anaongeza kuwa, mfano wa Bi Khadija (R.A.), mke wa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kielelezo cha mwanamke aliyekuwa kiongozi wa kiuchumi na kijamii katika zama zake.

Ni Dhahiri, uwezo wa mwanamke kuhudumia familia na mifano ya wanawake walioleta mabadiliko katika jamii kitaifa na kimataifa ni chachu ya kubomoa mitazamo hasi na mawazo mgando hususan katika zama hizi. 

Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii na Wazee Hassan Ibrahim Suleiman anafafanua kuwa, wanawake wana uwezo mkubwa wa kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali kuanzia familia, jamii hadi taifa endapo watapatiwa fursa sawa za elimu na uwezeshaji.

 Hata hivyo, amebainisha kuwa masharti ya ndoa ambapo baadhi ya waume huwazuia wake zao kushiriki katika shughuli za kijamii na kisiasa, ukosefu wa kipato cha kutosha unaosababisha utegemezi, na rushwa ya ngono, ni vikwazo vinavyowakwamisha wanawake wengi kufikia ndoto za kupata nafasi za uongozi.

Anasema, licha ya jitihada za serikali na taasisi binafsi, kuwekeza zaidi katika elimu ya wavulana kuliko wasichana, kwa dhana kwamba wanaume ndio tegemeo la familia. Anasisitiza kuwa uongozi ni mchakato unaohitaji harakati, muda na dhamira thabiti ambavyo kwa wanawake bado ni mwiba uliowasakama kutokana na majukumu ya kifamilia, mifumo dume na mitazamo hasi. 


Wataalam wa maswala ya kijamii wanaamini kuwa elimu ni chachu ya ujasiri, msimamo thabiti, na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika nafasi za uongozi. Hivyo, Mwanamke aliyeelimika huondokana na vizuizi vya fikra finyu na huchukua nafasi yake kama mshiriki kamili katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Kama anavyobainisha Kafui Adjamagbo-Johnson (2019, UN Africa Renewal) kwamba “Ukosefu wa wanawake kupata elimu bora, maarifa na rasilimali umekuwa kikwazo kinachowazuia kushika nafasi za uongozi barani Afrika.”


Katika kuimarisha mazingira rafiki ya kumwezesha mwanamke kufikia ndoto zake, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuimarisha usawa wa kijinsia katika elimu na kuhakikisha sera na mikakati iliyopo inawanufaisha wanawake kufikia safari ya uongozi na 50/50.

Tafiti kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZNZ zinabainisha kuwa tokea mwaka 2024 hadi 2025 imewawezesha takribani wanawake 11,600 na kujengea uelewa kwa masuala ya maamuzi na uongozi .

Ripoti ya Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Jinsia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-IGS) 2021, ilionesha kwamba elimu ya uongozi imekuwa chachu muhimu ya wanawake Zanzibar kujiamini na kuwania nafasi za kisiasa. 

Nunu Issa Juma, Makamu Mstaafu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), anaeleza kwamba elimu ina mchango mkubwa katika kumjengea mwanamke kujiamini. Amesema:

 “Kupitia elimu, nimepata ujasiri mkubwa wa kujieleza na kusimamia hoja zenye msingi.”

Anafafanua kuwa elimu humsaidia mwanamke kutetea haki na kushiriki katika mijadala ya kijamii na kitaifa kwa ufasaha zaidi. Elimu humwezesha kuelewa sheria na misingi ya haki za binadamu, hivyo kuweza kumlinda mwanamke dhidi ya kudhulumiwa.

Aidha, anasisitiza kuwa mafanikio ya mwanamke katika uongozi hayaji kwa bahati, bali kwa kujituma na kuwa na nia thabiti. “Wanawake wanaweza kuwa viongozi bora endapo jamii itabadilisha mtazamo kwamba mwanamke anaweza kuongoza.”amesema Nunu.

 Programu za kuwaandaa wanawake kuwa viongozi wa baadae katika vyuo vikuu ikiwemo Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) kupitia Dawati la Jinsia ni chachu ya inayowaelimisha pia kutambua haki zao na kujiamini katika kuchukua nafasi za uongozi.

Aidha, mchango Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa kushirikiana na TAMWA-ZNZ wamesaidia sana kukuza usawa wa kijinsia kuptia programu za uongozi kwa wanawake 

 Kila jamii inayothamini maendeleo huanza na uwekezaji katika elimu, humpa mwanamke uwezo wa kushinda vikwazo vya mila, desturi, na mitazamo duni inayomfanya aonekane asiye na uwezo wa kuongoza.

 Kwa kuzingatia nafasi kubwa ya elimu katika kubadilisha jamii, Aliyekuwa Raisi wa Afrika Kusini, marehemu Nelson Mandela (1994), amesema “Elimu ni silaha yenye nguvu zaidi ambayo unaweza kutumia kubadilisha ulimwengu.” 

Elimu ni nguzo muhimu inayompa mwanamke ujasiri, uelewa, na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika uongozi. Hata hivyo, elimu pekee haitoshi bila kujitambua na kuwa na maadili.

“Elimu pekee bila kujitambua haitoshi, uongozi unahitaji msimamo, maadili, na uthubutu wa kweli.”amesema Bikame.

Ili kufikia usawa wa kweli katika uongozi, jamii inapaswa kuendelea kuwekeza katika elimu ya wanawake, kuondoa vikwazo vya kijamii, na kukuza mitazamo chanya kuhusu uwezo wa mwanamke katika uongozi. Elimu ni msingi wa mabadiliko na daraja la kumuinua mwanamke kuwa kiongozi wa leo na wa kesho.

                                           MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...