HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA
Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi.
Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio
Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazini kuja nyumbani kushuhudia tukio hilo
Daktari dhamana wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Mkubwa Habib, amethibitisha kufikishwa mwili wa marehemu huyo hospitalini hapo na kuufanyia uchunguzi na kutoa wito kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kufahamu changamoto wanazopitia ili waweze kuzipatia ufumbuzi.
“Sasa hivi jamani kuna michezo mbali mbali kuna watu wanaigiza vitu vingi ambavyo vyengine ni vya hatari sana sasa kwa umri wa mtoto hawezi kupambanua kuwa yale ni maigizo, sasa wao wanayachukua yale kwenye Kichwa chake siku ikitokea kukerwa nae anafanya kama vile alivyoona kwenye TV” amesema
Katika tukio la pili tarehe 9.10.2025 mwandishi Siajabu Abdalla aliripoti tukio la mtoto mwenye umri wa miaka mitano (5) mkaazi wa Kikwajuni Mjini Magharibi Unguja kufariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya Kitambulisho.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi Abuubakar Khamis Ali, amesema tarehe 7.10.2025 saa 4:20 usiku huko Kikwajuni Gongoni mtoto mwenye umri wa miaka mitano aliyefahamikwa jina la ya Yassir Mohammed amekutwa ameshafariki dunia ndani ya chumba anacholala baada ya kujitundika kwenye msumari ulioko kwenye mlango wa chumba hicho kwa kutumia kamba ya Kitambulisho
Aidha Kaimu Kamanda huyo amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto wao ili kufahamu matatizo yanayowakabili.
Hali hiyo imeibua hoja na maswali mazito ambayo majibu yake hayakuweza kupatikana kirahisi, hivyo Wananchi wanaziomba Mamlaka za Serikali kufanya utafiti ili kugundua chanzo hasa cha matukio hayo ni nini ili jinamizi hili lisiendelee kuwakaba koo Wananchi Visiwani humo.
.jpg)
Comments
Post a Comment