WANAWAKE DARAJA LA WANAUME KUWA VIONGOZI KWENYE VYAMA VYA SIASA
MAKALA NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Mwaka 1992 Tanzania ilianzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa kutoka mfumo wa chama kimoja cha siasa ambacho kilikuwa ni TANU kilichokuwa kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julias K. Nyerere, na hapo ndipo utitiri wa vyama vipya vya siasa ukaanza hadi kufikia vyama 21, ambapo vitatu kati ya hivyo vikiwa vyama vikuu ambavyo ni Chama cha Mapinduzi-CCM Chama cha Demokrasia na Maendeleo –CHADEMA na Chama cha Alliance for Change and Transparency ACT Wazalendo. Ukubwa wa chama na ushindi unatokana na wingi wa wafausi ambapo wingi kwa kiasi kikubwa hupimwa katika mikutano ya Umma ya vyama ambapo asilimia kubwa ya wafuasi huonekana kuwa ni wanawake kuliko wanaume hususan vijana hilo hujidhihirisha kila kifikapo kipindi cha kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu. Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi - CCM wanakadiriwa kufikia 8,432,980 Tanzania huku idadi ya Wanawake ikikadiriwa kufikia 6,124,735 asilimia 68% kati ya wanachama wote, hii inadhi...