MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE
NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba linamshikilishia Ali Shavuai Ramadhan 25, ambaye ni mwalimu wa Madrasa anayeishi Wesha Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 14
Baba wa kambo wa Msichana
ambaye jina limehifadhiwa, amesema aligundua kuchelewa kurudi nyumbani kwa
binti yake huyo wakati wa usiku na kuchukua hatua za kumuuliza alikuwa wapi na
baada ya maswali kadhaa msichina huyo akajibu kuwa alikuwa mwalimu wake wa
madrasa nyumbani na kukiri kufanyiwa kitendo cha ubakaji
“Alichelewa kurudi
nyumbani akarudi kama muda wa saa 3 hivi nikamuita na kumuuliza ulikuwa wapi?
Akanijibu nilikuwa na mwalimu Ali nikamuuliza usiku mulikuwa munafanya nini na mwalimu
Ali? Akawa anasita kunijibu, nikaamuliza tena usiku mulikuwa wapi? Akajibu
nyumbani kwake, nikamuuliza mulikuwa munafanya nini? Baada ya muda kupita ndipo
akanijibu kuwa ni kweli wamefanya hicho kitendo zaidi ya mara moja” amesema baba mdogo wa
msichana huyo
Akieleza namna walivyotegua
mtego uliopangwa na familia ya mtuhumiwa ili kuivirigiza kesi hiyo, Baba mdogo
wa msichana huyo amesema “Tulipata taarifa kuwa binti yetu amefanyiwa vitendo
vya udhalilishaji na Ali Shavuai Ramadhani ambaye ni mwalimu wake wa madrasa lakini
wanapanga mpango wa kumpanga binti yetu amsingizie kijana mwengine ambaye ni
mdogo kiumri ili kesi hiyo ionde ke kwa huyo mwalimu na ihamie kwa huyo kijana
mdogo ili isiwe na uzito kwa kuonekana wote ni Watoto sisi baada ya kugundua
mpango moja kwa moja tukaenda kutoa taarifa Jeshi la Polisi na kushikiliwa wote
wawili huyo kijana aliyesingiziwa na huyo mwalimu lakini baadae yule kijana aliachiwa
baada ya kuonekana hakuna ishara ya kutenda kosa”
Mwandishi wa Habari hizi alifanikiwa
kuzungumza na msichana huyo ili kupata kauli yake dhidi ya tuhuma zakufanyiwa
vitendo hivyo vya ubakaji ambapo alikiri kufanyiwa kitenda hicho kwa nyakati
mbili tofauti na mwalimu wake
“Ni kweli tumefanya siku
mbili alikuwa anatutuma tukamchotee maji kisha tumpelekee nyumbani kwake sasa
kuna siku nilikwenda na mwenzangu kisha akamuambia mwenzangu ende zake kisha
nikabaki peke yangu tukafanya” amesema
Ndani ya kipindi cha miaka
miwili 2022/2024 hii ni kesi ya tano Kisiwani Pemba inayohusisha walimu wa
Madrasa kuwafanyia vitendo vya ubakaji wanafunzi wao.
Comments
Post a Comment