"BADO KUNA UNYANYASAJI MKUBWA WA KIJINSIA KATIKA VYAMA VYA SIASA" DK. MZURI
- Get link
- X
- Other Apps
Na, Hassan Msellem - Pemba
MKURUGENZI wa Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali, amesema bado Kuna vitendo vya unyanyasaji wa Kijinsia katika vyama vya siasa jambo linalosababisha Wanawake kukosa haki yao ya kuwa Viongozi.
Dk. Mzuri ameyasema hayo leo Oktoba 1, 2024 ukumbi wa mikutano wa chama hicho Tunguu Unguja, katika kikao na Wadau mbali mbali kujadili namna gani wanawake watapata ulinzi dhidi ya ukatili wa kijinsia mitandaoni, kupitia mradi wa wakuwawezesha waandishi wa habari vijana.
Amesema kuwa, katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kuna Ripoti kadhaa zinazoonesha unyanyasaji dhidi ya Wanawake waliotia nia nagombea nafasi mbali mbali za Uongozi ndani na nje ya chama Hali inayorudisha nyuma ndoto na juhudi za wadau katika kufikia azma ya 50 kwa 50 kwenye vyombo vya kutunga Sheria.
"Licha ya kazi kubwa inayofanywa na wadau katika kuhakikisha usawa wa Kijinsia unafikiwa katika vyombo vya maamuzi bado Kuna malalamiko makubwa kutoka kwa Wanawake wakilalamikia manyanyaso na vitosho kutoka katika vyama vyao hususan kipindi cha Uchaguzi" amesema
Dr. Mzuri pia amesema suala la unyanyasaji wa Kijinsia mitandaoni ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili Wanawake katika kutimiza ndoto zao zakushika nafasi mbali mbali za Uongozi na kusema "Kuna hili suala la unyanyasaji wakimtandao nalo ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili Wanawake wengi kutokufikia malengo kwani suala hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara na chakusikitisha zaidi Mamlaka ambazo zinajukumu la kukabiliana na suala hili zinaonekana kutokulipa kipaumbele katika kukabiliana nalo"
Aidha Dr. Mzuri amewataka Wanawake licha ya kukumbana na manyanyaso na vitosho kutokuogopa na badala ya kujiona upya kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 Ili kuongeza idadi ya Viongozi Wanawake katika vyombo vya kutunga Sheria.
Afisa kutoka Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhuhumu wa uchumi Zanzibar ‘ZAECA’ Yussuf Juma Suleiman, amesema moja kati ya vikwanzo vinavyowarudisha nyuma wanawake katika kugombea nafasi za uongozi ni rushwa ya ngono.
Amesema kuwa, kabla wanawake hawajaingia katika kugombea nafasi za uongozi, ni vizuri kupewa elimu ya uraia, ili kujua miiko na misingi ya uongozi, ili wasiwe na mwanya wa kutoa rushwa.
Aidha amesema kuwa, serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepitisha sheria mpya ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi, sheria namba 5 ya mwaka 2023, kifungu cha 53.
Amesema, kifungu hicho kimeharamisha rushwa ya ngono, kwa kukataza mtu yoyote kushawishi, kuahidi kufanya ngono na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka saba na kisichozidi miaka 10.
“Rushwa ya ngono ni uhalifu kama ulivyo mwingine, na serikali imeazisha sheria ili kukabiliana nayo, lakini wandishi wa habari toeni elimu ili wanawake wanaotia nia wasiwe ni mwanya wa kutokea rushwa,’’ alisema.
Nae Afisa sheria Mwandamizi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Abdul-razak Said Ali amesema serikali imekuwa ikichukua jitihada mbali mbali, katika kumuwezesha mwanamke kugombania nafasi za uongozi ili kuongeza ushiriki wao.
Alisema kuwa, moja ya hatua iliyochukuliwa na serikali ni kuongeza kifungu katika sheria ya vyama vya siasa nambari 1 ya mwaka 2024, kifungu namba 10 (c) ndani ya marekebisho, kinatoa masharti yanayohusiana na uanzishwaji wa dawati la kijinsia na ushirikishwaji wa jinsia na jamii.
Na washiriki wa mkutano huo Mwalim Mwatima Issa, Rashid alisema wandishi wa habari wanatakiwa kujipa kipaumbele katika kufanya kazi zao.
Nae mshiriki Nusra Shabani aliuliza kwanini vyama vidogo vya siasa, havipewi ruzuku ili kuviwezesha vishiriki kikamilifu katika uchaguzi.
Mwisho
Comments
Post a Comment