Skip to main content

WANAWAKE DARAJA LA WANAUME KUWA VIONGOZI KWENYE VYAMA VYA SIASA

 

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA




Mwaka 1992 Tanzania ilianzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa kutoka mfumo wa chama kimoja cha siasa ambacho kilikuwa ni TANU kilichokuwa kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julias K. Nyerere, na hapo ndipo utitiri wa vyama vipya vya siasa ukaanza hadi kufikia vyama 21, ambapo vitatu kati ya hivyo vikiwa vyama vikuu ambavyo ni Chama cha Mapinduzi-CCM Chama cha Demokrasia na Maendeleo –CHADEMA na Chama cha Alliance for Change and Transparency ACT Wazalendo.

Ukubwa wa chama na ushindi unatokana na wingi wa wafausi ambapo wingi kwa kiasi kikubwa hupimwa katika mikutano ya Umma ya vyama ambapo asilimia kubwa ya wafuasi huonekana kuwa ni wanawake kuliko wanaume hususan vijana hilo hujidhihirisha kila kifikapo kipindi cha kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi - CCM wanakadiriwa kufikia 8,432,980 Tanzania huku idadi ya Wanawake ikikadiriwa kufikia 6,124,735 asilimia 68% kati ya wanachama wote, hii inadhihirisha kuwa idadi ya wanachama wanawake ni kubwa kuliko wanaume

Katika za vyama mbalimbali vya siasa zinatoa haki sawa ya uanachama na uongozi kwa jinsia zote kwa mazingatio ya hoja ya kutumiza umri wa miaka 18 na kuwa mwanachama hai wa chama husika

Katiba ya ACT- WAZALENDO Ibara ya 8 (1) imesema “Uanachama wa ACT Wazalendo utakuwa kwa raia wote wenye umri wa kupiga kura bila ya kubagua jinsia,kabila,dini au hali yoyote, ibara hiyo inakwenda sambamba na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi Ibara ya 16 ambayo imeeleza kuwa “Kiongozi wa CCM ni kila mwanachama mwenye dhamira yeyote katika CCM aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba.

“Maoni ya Wananchi”

Maoni ya wananchi yanalenga kuwa jinsia ya kike kwenye vyama vya siasa hutumika tu kama daraja la wanachama na viongozi wanaume kufanikisha malengo yao ya kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya vyama na kulifanya kundi la wanawake kama wapiga debe na mtaji wa kisiasa.Jambo hilo linadhihirishwa na Rajabu Otham Ali,58 mkaazi wa Mgogoni Chakechake ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma -CHAUMA licha ya sheria zilizoweka wazi kuhusu suala la jinsia kwenye katiba za vyama vya siasa lakini suala hilo halijaweza kufikiwa kwa vitendo katika vyama vingi vya siasa nchini“Mimi niko kwenye siasa tangu mwaka 1980 na vyama vyote vina kanuni na katiba ambazo zinawaongoza ambazo zimezungumza vizuri kuhusu suala la usawa kijinsia ndani ya vyama lakini bado wanawake wanatumika tu kama mtaji wa viongozi katika vyama na ambaye anapata fikra za kugombea nafasi fulani anakubwa na vitisho hata kama ni mwana chama halali na ana uwezo” Amesema Rajab ambaye uzoefu wake unaonesha suala la wanawake kupewa nafasi ni si sehemu ya uhalisia wa katiba na kanuni za vyama vingi.

Wanawake ndio nguzo imara kwenye kampeni,kupiga kura na hata kwenye ushawishi kama ambavyo Aisha Ali Massoud 42, mama wa watoto 8 mkaazi wa Vitongoji Mchangani Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba ni mfuasi wa Chama Civil United Front -CUF kwa muda miaka 20 amesema viongozi wengi wakubwa wa vyama vya siasa nchini ni wanaume.“Nina miaka 20 ndani ya chama cha CUF na najitoa kwa hali na mali maana hata nyumba yangu muda mwengine hutumika kama tawi la chama lakini kujitoa kote huko sina nafasi yoyote na hata nikaitaka sidhani kama nitaipata maana naangalia hao wanawake wenzangu wanavyofanyiwa” Amesema Aisha ambaye kwake siasa ni maisha.

Hali ya kujiona mfuasi haiku kwa Aisha tu bali hali hii pia inaonekana kwa Nachia Ali Jamal 45, Mkaazi wa Shehia ya Wambaa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Mkoa wa Kusini Pemba kupitia Chama Cha ACT WAZALENDO ameendelea kutoa ushuhuda kuwa bado wanawake kwenye vyama vya siasa wana mchango mkubwa katika maendeleo ya vyama hivyo lakini umuhimu katika kushika nafasi za uongozi ndani ya chama ni jambo linalowekwa kisogoni.“Binafsi kinachonifanya niendelee kuwa mwanachama hai na kushiriki shughuli mbalimbali za chama changu ni kwasababu nimetoka nacho mbali sana tangu enzi za Mwalim Seif “ Nachia ameendelea kusema kuwa.”Ukweli kwamba bado wanawake hususan tunaoishi vijiji hatupewi fursa za kuwa viongozi kwenye chama na hizo nafasi tunazopewa ni zile tu ambazo wenyewe wanajua kuwa hatuwezi kuwa sehemu ya nguvu ya maamuzi ndani ya chama jambo hili ndilo linachangia wanawake kuwa madalali wa wanaume kwenye chaguzi”.Amemaliza Nachia.

“Viongozi wa vyama vya Siasa “

Suala la wanawake kutumia kama daraja na wenye ushawishi kwenye siasa linaweza linaonekana kuwa ni suala la kawaida ila viongozi wa kiasa wanaliona hili tofauti,Ashloo Massoud Khamis Katibu Mwenezi, Siasa na Mafunzo Wilaya ya Chake chake amesema elimu inayotolewa kwa vijana ndani ya CCM imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza usawa kijinsia kwasaabu wanawake wanapata elimu ya kutambua haki na wajibu wao.”Kwenye chama ukiangalia utagundua wanawake sasa wanashika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi za tatawi, wadi, Jimbo, Wilaya hadi Mkoa” Ashloo ameendelea kusema kuwa “Kwanza nikiri kuwa ni kweli wanawake ni wengi ndani ya chama kuliko wanaume na wanawake ndio tegemeo la chama chetu na CCM ndio chama kinachojali na kuzingatia usawa wa Kijinsia kuliko chama kingine chochote Tanzania,wanawake tunawapa nafasi katika chama chetu” Amemaliza Ashloo.

Lakini licha ya kuwepo kwa dhana ya wanawake kutumika kama daraja kwenye vyama vya siasa, vipo baadhi ya vyama ambavyo vimepiga hatua kuhusu suala la usawa wa kijinsia katika nafasi za Uongozi, Katibu wa Chama Cha ACT WAZALENDO Mkoa wa Chakechake kichama Saleh Nassor Juma amesema chama chao kinawathamini wanawake na kuwapata nafasi. “Nataka nikuhakikishe kama kuna chama ambacho kinajali, kuheshimu na kinazingatia usawa kijinsia ni chama chetu cha ACT Wazalendo kumbuka kuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo.

Ili kuondosha dhana ya utumwa kwa wanawake kwenye siasa wapo wadau mbali mbali ambao hukosa usingizi katika kuhakikisha wanawake nao wanakuwa viongozi katika Nyanja zote kuanzia ndani ya vyama vya siasa, taasisi binafsi na taifa kwa ujumla

Dina Juma Makota ni Mratibu wa Jumuiya ya Utetezi wa Kijinsia na Mazingira Pemba (PEGAO) amesema kupitia mradi wa Uhamasishaji Wanawake Katika Uongozi (SWIL) wamefanikiwa kuwafikia wanawake 1289 ambao wamehamasika na kujiunga na vyama vya siasa na kuweza kugombea nafasi mbali mbali ndani ya vyama vyao.

“Kupitia mradi wa SWIL tumeweza kuwafikia Wilaya zote za Pemba hususan Vijijini ambako ndiko kuna changamoto kuwa zinazowakabili wanawake kutokushiriki kwenye vyama vya siasa ambavyo ndio Daraja kuu la kuingia kwenye bahari ya Uongozi, hivyo basi ziara hizo zimeweza kuleta mabadiliko makubwa mno kwani tumeweza kuwafikia akina mama zaidi 1289 ambao wamepata muamko mkubwa na kuanza kujiunga katika jumuiya zao na vyama vya siasa na baadhi wameanza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ndani na nje ya vyama” amesema Mratibu wa Pegao



 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...