"WAHIMIZENI AKINA BABA KWENDA KILINIKI NA WAKE ZAO KWA MASLAHI YA AFYA YA MAMA NA MTOTO" BIKOMBO ABDALLA MASTUR

Na, Hassan Msellem, Pemba 

Wafanyakazi wa afya wa jamii (CHW) na Wauguzi wametakiwa kuwahamasisha akina mama kwenda kiliniki na wenza wao ili kuimarisha afya ya mama na mtoto.

Akifunga mafunzo ya siku kwa wafanyakazi hao afya wa jamii na wauguzi huko katika ukumbi wa Baraza la Mji Wete Bikombl Abdalla Mastur, Muuguzi dhamana Wilaya ya Wete na Mratibu wa huduma za Mama, katika ufunguzi wa mradi wa miaka miwili wa Kubadilisha Mtazamo wa Majukumu ya Kijinsia na Kuimarisha Maisha ya Wanawake na Wajawazito na Wanaonyonyesha katika familia za Vijijini Pemba unaondeshwa na Jumuiya kupunguza, amesema tafiti zinaonesha bado kuna ushiriki mdogo wa akina baba kuongozana na wake zao kwenda kwenye vituo vya afya hali inayosababisha maendeleo duni ya kiafya ya mama na mtoto.

Mratibu wa Jumuiya ya kupunguza umasikini na kuboresha Maisha ya watu Pemba (PEPOHUDA) Said Mbarouk Juma, amesema lengo la mradi huo ni kutoa elimu na kuwahamasisha akina baba kushirikiana na wenzao kwenda katika vituo vya afya ili kuimarisha afya ya mama wajawazito na mtoto.

Said Rashid Hassan, Mjumbe Jumuiya Pepohuda, amewataka wahudumu hao kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Afisa tabibu Kituo cha Afya Jadidi Wete Fatma Amour Hemed, amesema kituo cha Afya Jadidi kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi muhimu, uhaba wa wafanyakazi pamoja na gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) Hali inayosababisha kukosekana kwa huduma bora.

Farida Breki Karama, Muuguzi Mzambarauni, amesema Ili kuhakikisha idadi ya mama wajawazito wanajifungulia katika vituko vya afya wamekuwa wakitoa elimu katika jamii hasa maeneo ya Vijiji ambako ndiko kwenye idadi ya Akina mama wanaojifungua majumbani.

Mradi huo wa miaka miwili ambao umeanza mwezi July 2024 na kutarajiwa kukamilika Mwezi December 2026 unaendeshwa na Jumuiya ya kupunguza umasikini na kuboresha Maisha ya watu Pemba (PEPOHUDA) na kufadhiliwa na Shirika la Y+Global kupitia mfuko wa HER VOICE FUND



Comments

Popular posts from this blog

MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba

Mtangazaji wa Wasafi Media, Dida Afariki Dunia