AJALI YAUA WAANDISHI WA HABARI WAWILI WA MKOA WA LINDI.
WATU wawili ambao ni waandishi wa habari mkoa wa Lindi wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali .
Ajali hiyo iliyohusisha gari dogo imetokea majira ya usiku wa kuamkia Leo March 26 eneo la Nyamwage mkoani mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani)
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo Alli Husein alisema Waandishi hao walikuwa wanatokea Dar es Saalam kwenye mafunzo kurejea mkoani Lindi.
Waandishi waliofariki dunia ni Abdalla Nanda wa Chanel Ten mkoa wa Lindi na Josephine Kibiriti wa Sahara Media Group.
Matukio Daima media kumtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani)Protasi Mutayoka amethibitisha kutokea Kwa Ajali na kuwa Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 7 usiku wa March 26 na Chanzo ni Dereva wa Centar ambae baada ya ajali alikimbia na msako wa kumtafuta unaendelea.
Alisema kuwa kwenye gari ndogo ya waandishi walikuwa watu watatu na Wawili Mwanamke mmoja na mwanaume walifariki Dunia eneo la tukio na mmoja ni majeruhi amelazwa Hospitali na mguu wake mmoja amevunjika.
Kamanda huyo alisema eneo la ajali ni eneo nzuri Haina changamoto ya miundo Mbinu huku akitoa onyo Kwa madereva kufuata Sheria za usalama barabarani.
Chanzo. Matukio Daima.
Comments
Post a Comment