Wananchi waiomba Serikali kuweka vizuwizi barabara ya Pagali kueousha ajali.

 Salim Hamad,Pemba


Wananchi wa Shehia ya Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba,wameiyomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuifanyia maboresho njia ya kutoka Ikulu ya Pagali kueleke Pondeani na Wesha kutokana na kusababisha ajali za mara kwa mara.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo mara baada ya gari aina Ton hais kuacha njia na kuingia kwenye msingi ingawa hakuna aliyemajuri wala kupoteza maisha.

Msabah Said Mkaazi wa Tibirinzi amesema Njia hiyo ambayo haipiti mwezi imekuwa ikisababisha ajili kutokana na kuwepo kwa kibonde wakati wakuteremsha mlima huo.

Amesema mara nyingi gari au vyombo vya maringi mawili ndio vinaaongoza kwa kupata ajali kwa vile baada kushuka zinafeli breki na hatimai kuingia misingi jambo ambalo linaweza kuja kuleta maafa makubwa zaidi kama Serikali haikuchukua hatua.

‘’Tunaomba Seikali hii njia ya kutoka Ikulu Pagali kuifanyia marekebisha mana mlima ni mkubwa na huku chini kumefanya kibonde sasa wakati gari zikipta anataka kupinda kuelekea wesha mara nyingi zimekuwa zikifeli breki na hatimae kuingia misingini’’alisema.

‘’ili kuipusha kutokea maafa makubwa zaidi tunaishauri Serikali hile njia chini watujazie mchanga au wapitishe njia ilipokuwa imepita kuleza kwa zamani kabla ya kujengwa.

Fatma Khamis amesema wananchi wamaeneo hayo wamekuwa wakiishi kwa khofu kwa vile gari ziiaka njia zinakuja kwenye majumba yao.

Amesema suala hili linahitaji kuangalia kwa karibu ili kuepukana na madhara ambayo yanaweza kujitoza.

Afisa Mdhamini Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi Ibrahim Saleh Juma amesema wizara  itachukua hatua mbali mbali katika katika kuboresha miundombinu ya bara bara ili kuhakikisha inapunguza ajali zisizo za lazima.



Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba

Mtangazaji wa Wasafi Media, Dida Afariki Dunia