Waandishi wa habari chipukizi wapongezwa kwa kutendea haki mradi wa SWIL.

Na, Thuwaiba Habibu.

Mwenyekiti wa kamati ya utetezi kutoka Tamwa Bi shifaa said hassani amewapongeza waandishi wa habari chipukizi kutendea haki mradi wa wanawake na uongozi kwa kufanya kazi kwa kitaalamu zaidi.


Ameyasema hayo katika sherehe ya mahafali ya waandishi wa habari chipukizi yaliofanyika ukumbi wa bima mpira mkabala na kituo cha polisi madema alisema hawa waandishi wa habari chipukizi wameweza kutendea haki mradi wa wanawake na uongozi na kuweza kuibua vitu ambavyo walivisahau kama vipo katika jamii yao na kuweza kuviandikia makala za magazeti vipindi vya Redio na TV.


Alisema tumezoweya kuona makala zinazomuhusu mtu anahojiwa mtu mmoja peke yake lakini wao walitumia vyanzo tofauti tofauti vya habari na kazi zao ambazo amefanywa ziliandikwa kitaalamu kwani wengine kusubutu kutumia mikataba ya kikanda na kimataifa.


Pia aliwataka waandishi hao wasifanye mahojiano marefu ili kuleta ladha zaidi katika makala zao.


Alisema changamoto ambayo niliona ndani ya makala mulizofanya ni mohojiano marefu suala ambalo nimenifanya nijilazimishe kusikiliza na kusoma.


Aidha alisema kwa mwaka huu kidogo waandishi wamelisahau kundi la watu wenye ulemavu na kuwataka waandishi wajisongeze karibu na watu hawa kwani hizi ni sauti za wasio sauti.


"Hata kama hatukuwaweka katika makala zetu basi japo tuwafanyie mahojiano na wao wawe miongoni mwa walioshiriki alieleza"


Nae mjumbe wa bodi ya Tamwa bi Hawra shamte aliwaomba waandishi hao waweze kuwa ngangari na kutekeleza vigezo vyote vya uandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao Vizio ili kuhakikisha sauti za wanawake, vijana,watoto na watu wenye ulemavu zinasikika.


Alisema munatakiwa kuwa waadilifu na kufuata maelekezo ya uandishi wa habari na tusifanye kazi kwa kutegemea kitu na tufanye kazi kwa ajili ya kutetea jamii yetu.


Hata hivyo aliwashukuru wahariri na wasimamizi kuwasimamia kufanya utendaji kazi ulio imara.


"Mumeonesha kujitoa na kutuheshimisha kwa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi wanazo stahiki na naamini kuwa nyinyi ndio wahariri wa baadae"



Nao wahitimu wa mradi huo Berema Suleman Nassor na Nihifadhi Abdallah Issa walitowa shukurani kwa chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa kwa kuweza kuwapatia mafunzo yaliyoweza kuwafunza namna ya kuandika habari za wanawake na uongozi.


Awali walikuwa hawajuwa kitu gani wafanye katika kukamilisha kazi hii lakini kutokana na mafunzo waliopatiwa waliweza kujuwa kuandika hata kwa kutumia mikataba mbali mbali.


Vile vile walisema kuna changamoto mbali mbali walizokabiliana na lakini walihakikisha wanazishinda ili kukamiliza kazi hizo.


Comments

Popular posts from this blog

MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba

Mtangazaji wa Wasafi Media, Dida Afariki Dunia